Ubakaji wampeleka jela maisha
MKAZI wa Kata ya Igulubi wilayani Igunga mkoani Tabora, Sudi Seif (47), amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la ubakaji. Seif alihukumiwa jana na Mahakama ya Wilaya ya Igunga. Awali mwendesha mashitaka wa Serikali, Elimajid Emmanuel, akimsomea mashtaka ya mtuhumiwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Ajal Milanzi, alisema Aprili 16 hadi Juni 16 mwaka 2014, kwa nyakati tofauti, Seif aliwabaka na kuwaingilia kinyume na maumbile watoto wawili, mmoja mwenye umri wa miaka sita na mwingine tisa. Alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo na kuwasababishia maumivu makali watoto hao, jambo ambalo ni kinyume na kifungu cha 130, kifungu kidogo cha kwanza cha kanuni ya adhabu kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kinachozuia kutenda makosa kama hayo. Baada ya kusomewa mashtaka, Seif alikana kutenda makosa hayo na ndipo upande wa mashtaka ulipeleka mashahidi watano ambao walitoa ushahidi mahakamani. Baada ya kusikiliza ushahidi kut...