Nyama ya paka yamtia matatani

http://a3.urbancdn.com/w/s/ow/jqKJSDuetYdQdt-640m.jpg
MUUZA mishikaki mmoja katika kituo cha daladala cha Temeke mwisho jijini Dar es Salaam maarufu kwa jina la Said Mishikaki, amekamatwa na kupigwa na wananchi kwa tuhuma za kuuza mishikaki ya nyama ya paka.
Said alikamatwa jana asubuhi baada ya taarifa kusambaa katika eneo hilo zikimtuhumu kwamba amekuwa na kawaida kuuza mishikaki ya nyama ya paka badala ya ng’ombe, mbuzi na wanyama wengine wanaoliwa.http://www.funckr.com/genimg.aspx?fn=whatsup_1454.jpg&t=p&wp=5
Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, baada ya taarifa hizo kuenea, wananchi walilazimika kumtafuta muuza mishikaki huyo ili wamchukulie hatua.
Baada ya kumsaka kwa dakika kadhaa, hatimaye walifanikiwa kumkamata na kumkuta akiwa na paka mmoja aliyekuwa amemchinja na kumuweka kwenye ndoo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, wananchi hao walipomuona paka huyo akiwa amechinjwa, walichachamaa na kuanza kumshushia kipigo muuza mishikaki huyo na kumuumiza sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Kihenya Kihenya, alipozungumza na MTANZANIA kwa simu, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Hata hivyo, alisema taarifa za tukio hilo zinahitaji uchunguzi zaidi ili kuzithibitisha.
“Nilikwenda eneo la tukio na kukuta kielelezo cha mfuko wa nyama hiyo. Niliona nyama na utumbo mkubwa unaoonekana kama ni wa mnyama anayekula majani mfano wa ng’ombe.
“Inawezekana kuna matatizo katika biashara, huenda kweli ile ilikuwa nyama ya paka, lakini hatuna uhakika, hivyo tumechukua vipande vya nyama kwa ajili ya kuvipeleka kwa mtaalamu wa mifugo kwa uchunguzi zaidi ili kubaini aina hiyo ya nyama.
“Nyama hizo zilikuwa zinaonekana kubwa kama nyama za kuchemsha na utumbo ni mkubwa kama wa ng’ombe. Mimi nimeona haielekei kuwa ni ya paka. Kwa ujumla, hili jambo linahitaji uchunguzi zaidi,” alisema Kamanda Kihenya.
Pamoja na hayo, Kamanda Kihenya alionyesha kutoridhishwa kitendo cha wananchi hao kumpiga muuza mishikaki huyo.-Mtanzania

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4