Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MICHEZO

Azam yatia maguu dili la Mkude

Picha
AZAM imeamua kuingilia kati na kumshawishi kiungo wa Simba, Jonas Mkude aliyekuwa akinyemelewa na Yanga atue Chamazi, Mbagala. Mchezaji amebakiza miezi sita katika mkataba wake na Simba ambao bado hawajamuongezea ingawa tayari mazungumzo mepesi yameanza. Habari zilizopatikana jana Ijumaa zilieleza kwamba viongozi wa Azam walikuwa kwenye mpango wa kumalizana na kiungo huyo lakini hawakuweza kukamilisha mipango yao kwani Mkude yupo kambini na timu yake nje kidogo ya mji ikijiandaa na mechi yao na Ruvu Shooting itakayochezwa kesho Jumapili. Baadhi ya viongozi wa Simba jana walionekana kuhaha kuhakikisha wanafanya jitihada za kumbana mchezaji huyo ili asisaini mkataba na Azam ambapo wao wamepanga kumalizana naye baada ya mechi hiyo. “Azam wamepanga kumalizana naye na wapo tayari kwenda kumwingizia fedha kwenye akaunti yake, kinachochelewesha ni kwamba Mkude yupo kambini lakini kuna mazungumzo ya chinichini ambayo yamefanyika juu ya kumalizana na mchezaji huyo,” alisem...

Mosoti: Nipo tayari kurejea Simba

Picha
BEKI wa zamani wa Simba, Mkenya Donald Mosoti amesema yupo tayari kufuta kesi na kurejea Simba endapo tu watahitaji huduma yake na kufikia makubaliano kimkataba. Kauli hiyo aliitoa baada ya kuwepo na taarifa kwamba Kocha Patrick Phiri bado anamuhitaji beki huyo wa kati katika usajili wa dirisha dogo utakaoanza Novemba 15 ili kuboresha safu yake ya ulinzi ambayo inaonekana kuwa tatizo ndani ya kikosi chake. Jina la Mosoti lilikatwa siku mbili kabla ya dirisha la usajili mpya wa Ligi Kuu Bara kufungwa ambapo nafasi yake ilichukuliwa na mshambuliaji Mganda Emmanuel Okwi na hivyo kuamua kufungua kesi katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kesi ambayo inasimamiwa na wakili wake Felix Majani kwa madai ya kuvunjiwa mkataba wake pasipo makubaliano. Fifa iliwataka Simba kupeleka vielelezo vyao ikiwemo mkataba baina yao na Mosoti kwa ajili ya kuanza kusikiliza kesi hiyo kwa pande zote mbili lakini viongozi wa Simba walishindwa kufanya hivyo na Fifa sasa wanasubiri ku...

Mourinho happy with Costa's omission

Picha
Chelsea Head Coach Jose   English Premier League [EPL] side Chelsea Head Coach Jose Mourinho has confirmed that Diego Costa will feature against Liverpool on Saturday 8 November and thanked the Spanish Football Federation for omitting Diego Costa from the squad for their upcoming international fixtures. After consultation with Chelsea medical staff, Spain coach Vicente del Bosque omitted the Chelsea striker in the tactician's squad against Belarus set for Saturday 15 November in Euro 2016 qualifier and that of friendly match against world champions Germany three days later . Chelsea squad On the other hand Mourinho asserted that the forward who has been struggling with a hamstring injury since arriving at Stamford Bridge will feature against Liverpool at Anfield. -We think he is ready to start the match [on Saturday]. It is fantastic news for us. I thank the Spain FA for the decision that they made.The plan is to have a period of complete rest after the match for a f...

Usajili mpya wa Simba

Picha
KAMA ulitegemea kwamba Patrick Phiri anapigwa chini pale Simba umekosea. Tulia hapohapo usikie anachosema kiongozi mkuu wa Simba, Rais Evans Aveva. Amesisitiza kuwa hatamfukuza kocha huyo Mzambia na tayari amempa uhuru wa kuchagua wachezaji anaotaka kuwasajili kwenye dirisha dogo kwa gharama yoyote ile. Mbali na hilo pia amempa uhuru wa kuchagua wapi timu ikaweke kambi pamoja na mechi za kirafiki anazotaka kucheza wakati huu wa mapumziko ambapo usajili wa dirisha dogo utaanza Novemba 15 hadi Desemba 15. Aveva ameliambia Mwanaspoti kuwa mashabiki wengi hawakuelewa juu ya taarifa ya kumpa mechi mbili kocha Phiri haikuwa kumfukuza bali ni kuwaandalia taarifa ya kipi ameona ni tatizo na kupelekea timu yao kupata matokeo hayo ya sare mfululizo. “Hatuwezi kumfukuza kocha kwa matokeo hayo, tulimaanisha kwamba atuandalie ripoti ya kwa nini timu inapata matokeo haya na nini kifanyike, lakini pia tumempa uhuru wa kupendekeza majina ya wachezaji aliowaona kwenye ligi na ana...

Liverpool hoi kwa Real Madrid yalazwa 1-0

Picha
Katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imepigwa michezo minane ikiwemo ile ya mabingwa watetezi Real Madrid ambao wameinyuka Liverpool bao 1-0 kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid. Mfaransa Karim Benzema aliipatia Madrid bao hilo pekee baada ya kazi nzuri ya Marcelo. Katika mchezo huo kocha wa Liverpool Brendan Rodgers alifanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake kwa kuwaweka nje wachezaji wake muhimu saba akiwemo nahodha Steven Gerrard, Rahim Sterling na Mario Balotelli. Huko mjini London Arsenal wakiwa Emerates wameshindwa kulinda mabao yao pale waliporuhusu nyavu zao kutikiswa na kujikuta wakiambulia sare ya mabao 3-3 na Anderletch ya Ubelgiji. Hadi dakika ya 60 ya mchezo vijana hao wa Arsene Wenga walikuwa mbele kwa mabao 3-0 kabla wageni hao hawajacharuka na kurudisha mabao yote na kumuacha Wenga amefura kwa hasira. Kwingineko Borusia Dotmund wameikung’uta Galatasaray mabao 4-1, Juventus wakiiangushia kipigo cha 3-2 Olympiakos,kwenye mch...

Liverpool uso kwa uso na Madrid

Picha
  Madrid vs Liverpool Michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya inaingia mzunguko wa pili hii leo kwa mechi za marudiano ambapo mabingwa watetezi Real Madrid watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu kukipiga na Liverpool..ambayo katika mechi ya awali ilikubali kichapo cha fedheha nyumbani Anfield. Kocha wa Liverpool Brendan Rogers amesema hatomchezesha mshambuliaji wake Daniel Sturridge licha ya kusafiri naye hadi mjini Madrid kwa madai kuwa bado hajawa sawa kukabiliana na mechi kama hiyo…huku mwenzie wa Madrid Carlo Anceloti akisema leo anamrudisha kiwanjani Gareth Bale baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na kuwa majeruhi kwa mwezi mzima. Kwengineko Zenit St Petersburg ya Urusi itamenyana na Bayer Liverkusen ya Ujerumani, Arsenal itakuwa nyumbani Emerates wakiwakaribisha Anderletch ya Ubelgiji ilhali Juventus ya Italia wakikiputa na Olympiakos ya Ugiriki. Hapo kesho Manchester City watakwaruzana na CSKA Moscow ya Urusi dimbani Etihad,FC Bayen Munchen watachuana na AS...

Ngassa awa mfungaji bora Ligi ya Mabingwa Afrika

Picha
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa amepata zali Afrika, baada ya kumaliza kinara wa mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, licha ya klabu yake kuaga mashindano hayo alfajiri kabisa. Ngassa amemaliza kinara baada ya kufunga mabao sita na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif ya Algeria. Ni baada ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufikia tamati wikiendi iliyopita na ES Setif kutangazwa mabingwa wapya wakibebwa na bao la ugenini kutokana na matokeo ya sare bao 1-1 mchezo wa Algeria na sare mabao 2-2 mchezo uliochezwa Kinshasa. Ngassa aliyafunga mabao hayo katika raundi ya kwanza walipocheza na Komorozine ya Comoro mchezo wa kwanza walishinda 7-0 na marudiano walitoka kifua mbele kwa mabao 5-2. Yanga ilitolewa kwenye mashindano na Al Ahly ya Misri kwa penalti 3-4. Lakini Ngassa hawezi kupewa zawadi yoyote kwavile wamefungana na kiutaratibu hata mchezaji...

Suarez seeks first Barca goal at Ajax

Picha
Two defeats in as many games has not been the dream start Luis Suarez sought to life as a Barcelona player, but one of his old hunting grounds offers the chance to get up and running as the Catalans travel to Ajax on Wednesday. The Uruguayan scored 111 goals during a four-year spell with the Dutch champions before moving to Liverpool in 2011, but has yet to find the net since sealing his club record £75 million ($120 million, 96 million euro) move to Barcelona in July. Barca’s star-studded front three of Suarez, Neymar and Lionel Messi were denied by a fine goalkeeping display from Sergio Alvarez and the woodwork four times as Celta Vigo recorded their first away win at Barcelona since 1941 on Saturday, just a week after Barca were beaten for the first time in the league this season at Real Madrid. “The match against Ajax is the most important at the moment,” said Suarez, who played the full 90 minutes against Celta for the first time since his four-month ban for biti...

Walcott enters new contract talks

Picha
LONDON, England international Theo Walcott has entered contract negotiations with Arsenal after making a return from injury at the weekend. The 25-year-old winger will soon be entering the final 18 months of current deal, prompting the London outfit to begin talks over an extension to his reported £100,000 a week deal. Walcott featured as a substitute in Saturday’s Premier League victory over Burnley, making his long-awaited return after suffering a cruciate ligament injury at the start of the year. Commenting on Walcott’s contract situation, Gunners boss Arsene Wenger said: “We are starting to sit down with him. “I think he has one and a half years to go on his contract in December and it is never an easy job with him, you know.” He added: “Will he be at his peak in the next few years? He should be, yes. “He is 25. It is the best years now so hopefully we can profit from that.”- Tmedia

Arsenal na Mancity uwanjani leo

Picha
Mabingwa wa kombe la F.A nchini Uingereza Arsenal na mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchster City wanajianda kutoana jasho kuwania kombe la Charity Shield jioni ya siku ya jumapili. Mechi hiyo ndio itakayofungua rasmi msimu mpya wa ligi kuu nchini humo.   Mesut Ozil wa Arsenal Arsenal itajibwaga uwanjani ikiwa na wachezaji wapya waliosajiliwa kama vile Alexi Sanchez,lakini pia ikikumbuka kichapo cha mabao sita kwa tatu ilichopata dhidi ya mabingwa hao. Hatahivyo baada ya kushinda taji la F.A kuna motisha kubwa katika uwanja wa Emirates msimu huu. Yaya Toure Mancity Frank lampard aliyesaini kandarasi na kilabu ya Mancity kutoka Chelsea hatashiriki katika mechi hiyo . Vilevile hakuna mchezaji wa kilabu hiyo aliyewasili kutoka likizo ya kombe la dunia wiki iliopita ambaye atashirika katika mechi hiyo huku mshambuliaji Alvaro Negredo akiendelea kuhud...

Didier Drogba astaafu soka ya kimataifa

Picha
Drogba alisaidia nchi yake katika upatanishi baada ya mgogoro wa kisiasa Mchezaji soka maarufu wa Ivory Coast Didier Drogba, ametangaza kustaafu kutoka katika soka ya kimataifa. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, alichezea Ivory Coast zaidi ya mara miamoja. Alishiriki kombe la dunia mara tatu na mashindano ya kombe la Afrika mara 2 Amesema kuwa anajivunia kusaidia nchi yake kufika katika nafasi hiyo kimataifa. Drogba alipigia debe kumalizika kwa mgogoro wa kisiasa na pia kuhimiza pande zilizozozana kupatana.

Ghana katika hatari ya marufuku ya FIFA

Picha
Mashabiki wa Ghana Ghana inakabiliwa na tishio la kupigwa marufuku na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya serikali kuanzisha uchunguzi wa matokeo duni katika kombe la dunia huko Brazil. The Black stars ya Ghana ilimaliza na alama moja pekee katika kundi G baada ya kucheza mechi tatu . Aidha kampeini yao huko Brazil ilikumbwa na misukosuko ya nidhamu na migomo ya malimbikizi ya marupurupu ya wachezaji. FIFA imeipatia onyo shirikisho la soka la Ghana kuikumbusha kuwa inakiuka kanuni za shirikisho hilo kwa kuruhusu au kushiriki uchunguzi wa aina yeyote kuhusiana na matokeo duni katika mchuano wa kombe la dunia iliyofanyika huko Brazil.

Hatimaye Rodriguez apokea tuzo

Picha
Hatimaye James Rodriguez ametuzwa tuzo la mfungaji bora. Hatimaye mshambulzi wa Colombia James Rodriguez aliyeduwaza ulimwengu kwa kufunga mabao mengi zaidi katika kombe la dunia lililokamilika huko Brazil mwezi uliopita amepokea tuzo lake la mfungaji mabao mengi '' Golden Boot''. Rodriguez ambaye aliyetikisa wavu mara 6 huko Brazil sasa anakibarua cha kutafuta namba huko Real Madrid dhidi ya wakinzani wenye haiba yake kama mchezaji bora msimu huu Christiano Ronaldo. Rodriguez alinunuliwa na mabingwa hao wa kombe la mabingwa barani ulaya kutoka Monaco kwa pauni milioni 71. Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 23 alisema kuwa anamatumaini makubwa ya kutamba Santiago Bernabéu

Aliyepona Ebola akimbiwa na kutengwa

Picha
Aliyekufa kwa ebola azikwa Wakati virusi vya Ebola vikiendelea kusambaa katika Afrika Magharibi na kusababisha taharuki miongoni mwa wakazi wa nchi zilizokwisha kuathirika na ambazo bado hazijaathirika katika ukanda huo, baadhi ya walioupata gonjwa huo wamepona lakini pamoja na kupona bado hiyo haiwafanyi kukwepa kunyanyapaliwa. Mmoja ya wanafunzi wa udaktari ambaye amepona ugonjwa wa Ebola na kupewa cheti cha kuruhusiwa na kituo kilichokuwa kikimpa matibabu huko nchini mwake Guinea lakini amejikuta katika wakati mgumu kurudi katika maisha yake ya kawaida kwa kuwa watu wanamkimbia ikiwemo shule anayosoma wakimwambia abaki nyumbani. "Tunanyanyapaliwa na unajua wanapotutizama kama hivyo, unajua, hata familia yangu, watu wananitenga. Ninajisikia mpweke, wakati mwingine ninaenda matembezini. Ninaishi na Mjomba, wazazi wangu wanaishi kijijini. Nyumbani niko peke yangu, ninakula peke yangu na ninapohisi mambo hayako sawa ninaenda kutembeatembea. ...

Gerrie:Pistorius ni muongo wa kupindukia

Picha
Oscar Pistorius amejitetea kwamba alimpiga risasi kimakosa mpenzi wake Reeva Kiongozi wa mashtaka kwenye kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha mlemavu raia wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amemtaja mshtakiwa kama mtu aliyekolea uongo . Kwenye taarifa yake ya mwisho kiongozi wa mshataka Gerrie Nel amesema kuwa Pistorius aliumuua mpenziwe Reeva Steenkamp nyumbani kwake mjini Pretoria mwaka uliyopita. Bwana Nel alikataa taarifa kutoka kwa upande unaomtetea Pistorius kuwa mwanariadha huyo alimuaa mpenziwe kimakosa akidhania kuwa alikuwa ni jambazi aliyengia nyumbani kwake Mamake Reeva akiwa Mahakamani Wakili wa Pistorius naye alitoa taaraifa yake ya mwisho ambayo inatarajiwa kundelea pia kesho ijumaa akiwalaumu polisi kwa kuvuruga eneo kulikotokea mauaji. Baadaye mahakama hiyo itatoa umauzi wake wa mwisho kuhusu hatma ya mwanariadha huyo. Bwana Pistorius anatuhumiwa kwa mauaji ya mpenzi wake, Reeva Steenkamp, nyumbani kw...

Waaga dunia pamoja baada ya miaka 62

Picha
Don na Maxine Simpson wakiwa hospitalini Amini Usiamini mapenzi ya kweli bado yapo humu duniani! Kisa kimoja ambacho kimedhibitishia wengi baada ya wapenzi wawili waliooana na kuishi pamoja kwa takriban miaka 62 walipoaga dunia pamoja. Don na Maxine Simpson walikuwa wakazi wa mji wa Bakersfield, ulioko jimbo la California, Marekani waliaga dunia saa nne baada ya kushikana mikono hospitalini na kuahidiana penzi lao halitafifia kamwe hata mauti iwapate. Walikuwa wamelazwa hospitalini kufuatia hali duni ya afya inayotokana na umri wao mkubwa Don na Maxine Simpson wakiwa bukheri wa afya Lakini punde alipoaga Maxine na mwili wake ukaondolewa chumbani walikokuwa wamelazwa pamoja na mumewe Don, zilipata saa nne tu uchungu ulipomzidi Don na akakata roho iliwaendelee kupendana na mkewe ahera. Mjukuu wao Melissa Sloan aliiambia runinga ya KERO-TV Kuwa Don alimhusudu sana nyanya yake yaani Maxine tangu al...

Bobby Williamson amepata kibarua kipya kenya

Picha
Kocha mpya wa Harambee Stars Bobby Williamson Kocha wa Gor Mahia Bobby Williamson amechaguliwa kuwa kocha wa Harambee Stars ya Kenya baada ya Adel Amrouche kufutwa kazi siku ya Jumapili kufuatia kushindwa kwa Kenya katika raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Lesotho. Williamson ambaye aliwahudumu kama kocha wa Uganda Cranes kwa miaka mitano kabla ya kutimuliwa baada ya Cranes kushindwa kufuzu kwa kombe la mabingwa barani Afrika CAF mwaka wa 2013 amesema kuwa ni jambo la kujivunia kuteuliwa kuwa kocha wa timu ya Harambee Stars . Hata hivyo raiya huyo wa Scotland amesema kuwa bado ataendelea na majukumu yake katika klabu mabingwa wa ligi kuu ya Kenya KPL hadi pale shirikisho la soka la Kenya FKF litakapokubaliana na klabu yake ya Gor Mahia. Williamson anatarajiwa kuiongoza Gor mahia katika mchuano wa baraza la soka kanda ya Afrika Mashariki na Kati baada ya kutwaa taji la taifa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 18....

Xavi Hernandez astaafu soka

Picha
Kiungo wa Barcelona na Spain Xavi Hernandez ametangaza kustaafu soka la kimataifa. Hernandez mwenye umri wa miaka 34 alichezea timu yake ya spain na kutwaa ushindi na pia makombe mawili ya champion Ulaya akiwakilisha nchi yake. Xavi amewaambia waandishi wa habari Barcelona jumanne hii kuwa anafuraha kutimiza kipindi chote cha kucheza soka hadi anapofikia kustaafu na kwamba kwa kipindi chote hicho amekuwa na wakati mzuri. Akiwa na umri wa miaka 20 alianza kung'ara baada ya kuipatia ushindi timu yake katika mechi ya 15 November 2000 ambapo Netherlands ililazwa bao1-0 dhidi ya Spain. Katika umri huo pia Xavi alikaririwa na vyombo vya habari akisema mie si mwenye miaka 20 tena lakini bado nina hamasa ya kitoto. Hata hivyo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2008 katika ligi ya ulaya wakati huo Hispania ikiwa inasubiri kutwa kikombe ch...

S.Leone yapiga marufuku Kandanda

Picha
Mechi za soka zapigwa marufuku nchini Sierra Leone. Shirikisho la soka la Sierra Leone limepiga marufuku mechi zote za kandanda nchini humo ikihofia kuenea zaidi kwa maradhi ya homa ya Ebola. Hatua hiyo inafuatia marufuku iliyotangazwa na rais Ernest Bai Koroma katika jitihada za kuzuia kuenea zaidi kwa maradhi ya ebola nchini humo. Hali hiyo ya tahadhari iliyotangazwa na rais inatarajiwa kudumu kwa kipindi cha siku 60 hadi 90.   S.Leone ilikuwa inatarajiwa kuikaribisha Cameroon mwezi ujao Kufuatia marufuku hiyo huenda taifa hilo likakosa kuandaa mechi ya kufuzu kwa dimba hilo dhidi ya timu ya taifa na Cameroon iliyokuwa imeratibiwa kuchezwa mwezi ujao. Aidha maandalizi ya mechi ya ufunguzi ya kundi D dhidi ya Ivory Coast inatarajiwa pia kuathirika. Marufuku hiyo pia itaathiri pakubwa maandalizi na mechi za mkondo wa pili wa ligi ya Sierra Leone. Timu ya Sierra Leone imekuwa nchini Kenya kwa...

Yanga yashusha mastaa Kagame,yamzuga Kiiza

Picha
KOCHA wa Yanga, Mbrazili Marcio Maximo ameamua kuwatupia mzigo wa Kombe la Kagame wasaidizi wake, Leonardo Neiva na Shadrack Nsajigwa na kuwapa wachezaji 21 ambao anasema wana uwezo wa kurejea na kombe hilo Tanzania Lakini watani wa Yanga baada ya kusikia uamuzi wa Maximo wakaanza kukejeli kwamba amekimbia lawama ingawa yeye ameeleza wazi programu yake. Wakati Neiva na Nsajigwa wakienda kupambana nchini Rwanda Maximo ataungana na kocha wa kikosi cha timu ya vijana ya klabu hiyo, Salvatory Edward kuweka kambi Pemba. Yanga imepangwa kundi A katika michuano hiyo na itatupa karata yake ya kwanza  Agosti 8 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda. Japo Maximo amefanya siri juu ya kikosi kitakachokwenda kwenye kombe la Kagame, Mwanaspoti linafahamu kuwa wachezaji walioko na timu za taifa ni Oscar Joshua na Nadir Haroub Cannavaro pekee watakaoungana na kikosi hicho. Oscar anapewa nafasi kubwa ya kwenda kutokana na nafasi anayoicheza kuwa na mchezaji mmoja tu Amosi Abel...