Ni yapi yaliyojitokeza Davos?
Mawaziri kutoka nchi 75 zikiwemo Marekani na China wamekubaliana kuanzisha mazungumzo juu ya kanuni za kimataifa za uendeshaji biashara mtandaoni katika shirika la biashara duniani WTO. Mazungumzo hayo yametangazwa na afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya Cecilia Malmstrom, pembezoni mwa kongamano la dunia la kiuchumi linalomalizika Ijumaa mjini Davos, ambako viongozi wa dunia walikuwa wakipinga suala la ulinzi wa viwanda unaopigiwa upatu na Marekani. Tangazo hilo lililopitsishwa karibu na nusu ya wajumbe wa shirika la biashara WTO, ni ushindi wa nadra katika ushirikiano wa kimataifa, wakati Beijing na Washington zikiwa katika vita vya kibiashara. Trump amelituhum shirika hilo kwa kutojali maslahi ya kibiashara ya Marekani dhidi ya China. Mazungumzo hayo yataanza rasmi mwezi Machi, na kujaribu kuweka urahisi na usalama katika "ununuzi na uuzaji wa vitu kupitia mtandaoni". Naye mkuu wa benki ya dunia Kristalina Georgieva amewataka wa...