Baba amchoma mdomo mwanaye, kisa maharage
POLISI mkoani Kigoma wanamshikilia Sindotuma Nyamubi
(39) wa Kijiji cha Kasaka Kata ya
Nyaruyoba Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma akidaiwa kumchoma moto na kumuunguza mdomo mtoto wake
baada ya kumtuhumu kudokoa maharage
jikoni.
Ofisa Mtendaji wa
Kijiji hicho, Felix Cosmas, alisema baada ya kumuunguza alimfungia ndani
mtoto huyo kwa siku tatu na ndipo ilipobainika kwa majirani kutokana na
kutoonekana akicheza na wenzake nje hivyo kutoa taarifa polisi na mzazi huyo
alikamatwa.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kibondo, Michael Joshua, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kumtaja
mtoto aliyefanyiwa unyama huo na mazazi wake kuwa ni Shukuru Sindotuma na baada
ya mtuhumiwa kufikishwa kituoni hapo alikiri kumchoma mtoto wake mdomo kwa kula maharage bila ya ruhusa yake.
Maoni
Chapisha Maoni