Moto waunguza bweni ya Musoma Utalii
BWENI moja la wasichana la Shule ya Sekondari ya Musoma Utalii
katika kijiji cha Nyabange nje kidogo ya
mji wa Musoma mkoani Mara, limeungua kwa moto na kuteketeza vitu mbalimbali vilivyokuwamo.
Makamu Mkuu wa
Sekondari hiyo, Baraka Julius, alisema moto
huo ulitokea juzi mchana kutokana na
hitlafu ya umeme lakini kwa jitihada za wanafunzi na wananchi waliendelea
kuuzima mpaka gari la kikosi cha Zimamoto lilipowasili.
Alisema jitihada za awali za kuzima moto zilizofanywa na wanafunzi
wenyewe zilifanikiwa kwa kiasi na
kusaidia kuokoa baadhi ya mali zao ingawa nyingine ziliteketea.
“Ni vugumu
kusema kiasi sahihi cha mali kuteketea
kwa kuwa hatujafanya tathmini sahihi ya
janga hili la moto. Tunachoshukuru ni
kuwa bweni hili limeungua wakati wanafunzi wakiwa wanaendelea na vipindi
darasani,” alisema Baraka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Philip Kalangi
alithibitishwa kutokea kwa moto huo na kusema hakuna vifo vilivyotokea.
Chanzo cha moto huo hakijajulikana na polisi
kwa kushirikiana na Zimamoto wanaendelea kufanya uchunguzi.
Maoni
Chapisha Maoni