Taarifa mpya kuhusiana na stori ya Mishikaki ya paka
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Polisi Temeke, Kihenya Kihenya amesema
sampuli ya nyama inayodaiwa kuwa ya paka imekabidhiwa kwa mtaalamu wa mifugo kuifanyia
uchunguzi.
Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Kamanda Kihenya alisema
nyama hiyo imekwisha kukabidhiwa kwa
mtaalamu wa mifugo kuifanyia uchunguzi kwa
vile nyama hiyo imewatia wasiwasi baadhi
ya wananchi.
Juzi wananchi walimpiga kijana mmoja, Said Mishikaki, kwa madai ya kuwauzia nyama ya
paka katika Kituo cha Daladala cha Temeke Mwisho.
Muuzaji huyo wa mishikaki
anadaiwa kuwa amekuwa maarufu kwa jina hilo kutokana na uzoefu wake katika kuuza mishikaki ambayo wateja wamekuwa
wakiikimbilia.
Kamanda Kihenya alisema wanataka sampuli hiyo itabidi ichunguzwe kuondoa
wasiwasi kwa wananchi wa eneo hilo.-Mtanzania
Maoni
Chapisha Maoni