Dawa zilizopigwa marufuku zauzwa Dar
BAADHI ya maduka Jijini Dar es saalam yanaendelea kuuza dawa zilizofutiwa
usajili na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) baada ya kubaini zina madhara kwa binadamu.
Mamlaka hiyo ilifuta usajili kwa aina tano za dawa ya vidonge ya kutibu
fangasi kasuli(ketoconazole), dawa ya kutibu malaria ya maji na vidonge
Amodiaquine (monotherapy).
Dawa nyingine zilizofutiwa usajili na kupigwa marufuku kuuzwa
madukani ni pamoja na ya kutibu mafua na kikohozi ya maji na ile ya vidonge pamoja
na kapsuli zenye kiambato hai (phenypropanl amine).
Dawa nyingine ni ile ya kuua bacteria ya sindano (chloramphenicol
sodium) na dawa ya kuua bacteria ya maji pamoja na kapsuli(Cloxacillin).
MTANZANIA ilitembelea baadhi ya maduka ya dawa maeneo ya Mabibo, katikati
ya jiji, Ubungo Maziwa na Mwenge na kukuta dawa hizo zikiendea kuuzwa.
Akizungumza hali hiyo jana, Ofisa Habari wa TFDA, Gaudensia Simwanzi
alisema kwa sasa wataalamu wa mamlaka hiyo wapo katika ukaguzi unaofanyika sehemu
mbalimbali nchini.
Alisema kuna mtandao unaoendelea kufanya ukaguzi sokoni kwa sababu baadhi
ya wafanya biashara sio waaminifu kwani wanaendelea kuuza dawa hizo
“Dawa ya SP iliyo kuwa ya malaria
imebadilishiwa matumizi sasa inatumika kama kinga ya malaria kwa
wajawazito tu, dawa hii inatakiwa kupatikana hospitali na zahanati tu, hivyo kwenye
maduka ya dawa hazitakiwi kuwemo kuanzia sasa.
“Tunawahakikishia watumiaji hakutokuwapo tena na dawa hizo sokoni
tupo kwenye ukaguzi,”alisema Simwanzi.-Mtanzania
Maoni
Chapisha Maoni