Maduka Dar yazidi kuuza dawa zenye madhara
BAADHI ya maduka Dar
es saalam yameendelea kuuza dawa zilizo
futiwa usajili na Mamlaka ya
Chakula na Dawa(TFDA) baada ya kubaini zina madhara kwa binadamu.
TFDA ilifuta usajili
wa aina tano za dawa ambazo ni dawa ya kutibu fangasi ya vidonge na
kasuli(ketoconazole) na dawa ya kutibu
malaria ya maji na vidonge Amodiaquine (monotherapy).
Dawa nyingine zilizopigwa marufuku kuuzwa madukani ni dawa ya
kutibu mafua na kikohozi ya maji na ile ya vidonge na kapsuli zenye
kiambato hai (phenypropanl amine), dawa
ya kuua bacteria ya sindano (chloramphenicol sodium) na dawa ya kuua bacteria
ya maji na kapsuli(Cloxacillin).
Mtanzania ilitembelea baadhi ya maduka ya dawa Mabibo, katikati ya jiji na Ubungo Maziwa
na kukuta yanaendelea kuuza dawa zilizofutiwa usajili.
Ofisa Habari wa TFDA, Gaudensia Simwanzi alisema, “kwa sasa tupo kwenye ukaguzi sehemu
mbalimbali nchini katika maduka yote ya dawa.
“Dawa ya SP iliyokuwa ya malaria imebadilishiwa matumizi sasa inatumika kama
kinga ya malaria kwa wajawazito tu.
“Dawa ya SP inatakiwa kupatikana katika hospitali na zahanati tu, hivyo hazitakiwi kuwapo kwenye maduka ya dawa kuanzia
sasa,”alisema Simwanzi.
Maoni
Chapisha Maoni