Tusiime yang’ara kidato cha nne
SHULE ya Sekondari Tusiime ya Tabata Dar es Salaam,
imeendeleza umwamba wake katika matokeo ya kidato cha nne ambapo wanafunzi 90
wamepata ufaulu uliojipambanua.
Tusiime secondary school |
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa mwishoni mwa
wiki na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), wanafunzi wengine 98 wa shule
hiyo wamefaulu vizuri na hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyepata daraja la
mwisho.
Matokeo hayo yanaonyesha shule hiyo imefanikiwa
kushika nafasi ya tano kimkoa kati ya shule 191 na imeongoza somo la kemia
kati ya shule 397 mkoani Dar es Salaam na imekuwa ya tano kitaifa kwenye somo
hilo.
Vile vile imekuwa ya tatu kimkoa katika somo la
biashara kati ya shule 311 na ya 11 kitaifa kwa somo hilo kati ya shule
1,241.
Aidha, katika somo la fizikia kimkoa imekuwa ya
nne kati ya shule 393 ya nane kimkoa katika masomo ya Jiografia na Book
Keeping na kwa matokeo ya jumla imekuwa ya tano kwa Mkoa wa Dar es Salaam
kati ya shule 191, huku kitaifa ikiwa ya 41 kati ya shule 2,322 katika kundi
lenye watahiniwa zaidi ya 40.
Kwa matokeo hayo kati ya wanafunzi 208 waliofanya
mtihani huo, wanafunzi 90 wamepata daraja la kwanza, 98 daraja la pili na 20
daraja la tatu na hakuna daraja la nne wala 0.
Akizungumzia matokeo hayo, Mkuu wa shule hiyo,
Emil Rugambwa, aliwapongeza walimu wake kwa kazi na jitihada kubwa
walizofanya kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kama hayo.
Akizungumzia siri ya ufaulu huo mmoja wa wanafunzi
aliyepata GPA ya 4.6, Antony Mataro,
ambaye mwaka 2012 akiwa kidato cha pili aliongoza kitaifa kwa kupata alama A
kwa masomo yote.
Maoni
Chapisha Maoni