Wivu: Mwanaume amuua mkewe kwa kumchoma kisu

MWANAUME mmoja, George Mnyiramba (45), mkazi wa Kijiji cha Kawaya, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, amemuua mkewe, Farida Mnyiramba (40), kutokana na wivu wa mapenzi.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Novatus Makunga, aliliambia MTANZANIA jana kwamba, mwanaume huyo alimuua mkewe huyo kwa kumchoma visu katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.
Makunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, alisema mauaji hayo yalitokea Februari 17 mwaka huu saa tano usiku.
“Baada ya mtuhumiwa huyo kutenda kosa hilo, alikunywa sumu ya kuulia magugu shambani lakini hakufanikiwa kupoteza maisha kwa sababu alikimbizwa hospitalini na kupatiwa matibabu.
“Kwa hiyo uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini ukweli juu ya tukio hilo ili hatua mbalimbali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake,” alisema Makunga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa huyo kwa uchunguzi zaidi.
Pamoja na hayo, alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Hai ukisubiri taratibu za mazishi kufanyika.-Mtanzania

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4