TMA yatahadharisha mvua kubwa yaja
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)imetoa tahadhari kwa wakazi wa
maeneo ya mabondeni kuhama kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika baadhi ya mikoa
nchini.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa TMA,
Dk.Agnes Kijazi alisema hali ya hewa kwa sasa si nzuri na inasababisha hofu kwa
wakazi wanaoishi mabondeni.
“Kutakuwa na upepo mkali utakaoendana na ngurumo za radi hali
itakayosababisha kujaa maji katika baadhi ya maeneo na kuleta athari
za mafuriko kwa wakazi wanaoishi mabondeni.
“Mikoa ambayo mvua imeishaanza kunyesha ni ya
Nyanda za Juu Kusini ikiwamo Mbeya,Iringa na Rukwa na bado baadhi ya mikoa mvua
hii imeanza kunyesha.
“Ni bora wananchi wachukue tahadhari mapema kuliko kusubiri athari itokee,”alisema
Kijazi.
Pia mkurugenzi huyo alitahadharisha watumiaji wote wa bahari kuwa
makini wanapokuwa maeneo ya fukwe kulingana na hali ya hewa ilivyo sasa na siku zinazoendelea na mamlaka
itandelea kutoa taarifa kulingana na hali halisi.
Maoni
Chapisha Maoni