Raia wa kigeni wakamatwa na madini JNIA
RAIA wa kigeni wanaofanya biashara haramu ya madini wamekamatwa na
madini yenye thamani ya Dola za Marekani 113,807.11 sawa Sh milioni 641.853 katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa
Fedha na Utawala wa TMAA, Bron Mteta alisema watu hao walikamatwa katika
matukio 27 tofauti huku wakiwa na madini ya aina mbalimbali.
Alisema miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na lile la Juni 12 mwaka
jana ambapo raia mmoja alikamatwa kwenye uwanja huo akiwa na madini ya vito vyenye
uzito wa gramu 1,290 yenye thamani ya dola za Marekani 11,591.82.
Alisema mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na kuhukumiwa adhabu ya
kulipa faini ya Sh 300,000.
Alisema katika tukio jingine la Desemba 14 mwaka jana,raia mwingine
wa kigeni alikamatwa kwenye uwanja huo akiwa na madini ya vito ya uzito wa
karati 288 na thamani ya dola za Kimarekani 23,235.50.
Alisema mpaka sasa hatua za kisheria zimechukuliwa kwa mtuhumiwa
huyo ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani na kupewa adhabu ya kulipa faini
ya sh.500,000.
Maoni
Chapisha Maoni