MBUYU Twite ameanza kuona chungu ya kugombana na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans van der Pluijm baada ya jana kutupwa nje ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo inayojiandaa kucheza na Ruvu Shooting leo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utakuwa ni muhimu mno kwa Yanga kwani iwapo itashinda, itakuwa imejisogeza karibu zaidi na ubingwa wa ligi hiyo na itafikisha pointi 52, ikibakiza pointi tatu kutangaza ubingwa. Azam ndiyo wanaoshika nafasi ya pili katika ligi hiyo wakiwa na pointi 42, wakiwa wamebakiza mechi nne na iwapo watashinda zote, watafikisha pointi 54. Na kuelekea mchezo wa leo wa Yanga, kikosi hicho jana asubuhi kilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ambapo Twite hakuwapo katika kikosi cha kwanza. Kikosi hicho cha kwanza cha leo kiliundwa na kipa Ally Mustapha ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Kelvin Yondani, Said Juma, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Kpah ...