Hazard mchezaji bora wa mwaka England
Baada ya kusubiri kwa misimu
miwili hatimae Eden Hazard wa Chelsea ameibuka mchezaji bora wa mwaka
wa England na kutwaa tuzo ya PFA.
Hazard mwenye umri wa miaka 24
amefunga mabao 13 na na kusaidia wafungaji (assists) 8 katika michezo 33
ya ligi kuu ya nchi hiyo na kuisaidia timu yake kushika ususkani katika
msimamo wa ligi.
Naye Harry Kane mwenye umri wa miaka 21 ameibuka
kidedea kwa kunyakua tuzo ya mchezaji bora chipukizi huku naye Ji
So-Yun wa Chelsea akiibuka mshindi kwa upande wa wanawake.
Hazard
ambaye msimu uliopita aliibuka mshindi kwa upande wa chipukizi
alikabidhiwa tuzo yake katika hoteli ya Grosvenor jijini London jana
Jumapili. " ninafuraha sana. Nataka siku moja niwe mjichezaji bora
kabisa na na nilichofanya msimu huu ni kucheza vizuri na timu yangu
imecheza vizuri sana" alisema Hazard baada ya kupokea tuzo hiyo. "sijui
kama nastahili kushinda lakini jambo hili ni zuri kwangu. Ni jambo zuri
kupigiwa kura na wachezaji kwasababu wanajua kila kitu kuhusu mpira"
aliongeza mchezajia huyo.-bbc
Maoni
Chapisha Maoni