Mwili wa mwanafunzi alichapwa viboko wawasili Dodoma
MWILI wa
mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Matui iliyoko Wilaya ya
Kiteto, Mkoa wa Manyara, aliyedaiwa kufariki baada ya kuchapwa viboko na walimu
wake, Emmanuel Mbigima (15), umefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Dodoma.
Wakati mwili
huo unafikishwa hospitalini hapo jana asubuhi, ulikuwa umewekwa kwenye gari la Halmashauri
ya Wilaya ya Kiteto ukisindikizwa na baadhi ya ndugu wa karibu wa familia ya
marehemu.
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, babu wa marehemu, Emmanuel Ngowi, alisema mwili huo umeletwa hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ambavyo vimekosekana katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto.
"Mjukuu wangu alipigwa na walimu watatu tarehe 20 mwezi huu kutokana na kufeli mtihani wa somo la Kiswahili.
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, babu wa marehemu, Emmanuel Ngowi, alisema mwili huo umeletwa hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ambavyo vimekosekana katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto.
"Mjukuu wangu alipigwa na walimu watatu tarehe 20 mwezi huu kutokana na kufeli mtihani wa somo la Kiswahili.
“Tumechukua
uamuzi wa kumleta hapa kwa sababu madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto,
walishindwa kubaini kichwa kimeathirika kwa kiasi gani kwa kuwa hawana vifaa
vya uchunguzi vya kichwa.
“Hata hivyo, majibu
ya uchunguzi wa awali yaliyotolewa katika hospitali hiyo, yalionyesha
jicho la kulia lilivuja damu kwa ndani na pia mwili wa marehemu ulikuwa na
michubuko miguuni,” alisema Ngowi.
Naye mjomba wa
marehemu, Michael Ezekiel amesema matukio ya wanafunzi kupigwa na kupoteza
maisha yamekuwa yakijirudia shuleni hapo kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa
dhidi ya watuhumiwa.
“Mwaka jana
kuna mtoto alipigwa na mwalimu akafariki, lakini mtuhumiwa alipelekwa
mahakamani na baadaye kuachiwa kwa madai kuwa mtoto alikuwa ni mgonjwa,” alisema.
Kwa upande
wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk. Zainabu
Chaula, alithibitisha kupokelewa kwa mwili huo na kusema uchunguzi bado
unaendelea.
Awali, akizungumza baada ya mwanafunzi huyo
kufariki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime, aliwataja
walimu waliohusika katika tukio hilo na ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi,
kuwa ni Machael Bajutta (28), Chalamilla Gereza (33) na Mwalimu Joyce Msiba
(36).
Maoni
Chapisha Maoni