Mgodi wa Buzwagi kufungwa
MAKAMU
wa Rais wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Acacia, Deo Mwanyika, amesema mgodi
wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga utafungwa
kutokana na uzalishaji kushuka.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mwanyika amesema mashapo ya dhahabu ya mgodi wa
Buzwagi yana uwezo wa kutoa Ounce 900,000 ya dhahabu yenye ubora wa gramu 1.35
kwa tani hivyo kudumu kwa kipindi cha miaka mitano.
Amesema
kutoka na hali hiyo, uongozi wa Kampuni ya Acacia utalazimika kuufunga mgodi
huo na kuelekeza nguvu kwenye migodi ya Bulyankhulu na North Mara.
Amesema
upande wa mgodi wa North Mara uliopo Wilaya ya Tarime, unao uwezo wa kutoa
Ounce milioni 2.02 ambazo zina ubora wa gramu 2.6 kwa tani moja.
Amesema
mgodi wa Bulyankhulu una kiasi kikubwa cha mashapo yenye uwezo wa kutoa Ounce
milioni 9.2 ambazo zina ubora wa gramu 9.7 kwa tani moja hivyo kukadiriwa kuwa
na muda mrefu wa kuendelea na uzalishaji kwa miaka 40 hadi 60 ijayo.
Alisema
kutokana na kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la dhahabu duniani, migodi
yote ya Acacia imeanza kujielekeza kupunguza gharama za uzalishaji.
Katika
hatua nyingine, amesema Kampuni ya Acacia imefanikiwa kulipa Sh bilioni 2.2 za
ushuru wa huduma kwa halmashauri za wilaya ya Tarime mkoani Mara, Msalala na
Kahama mkoani Shinyanga kuanzia Juni
hadi Desemba, mwaka jana.
“Tulilipa ushuru wa huduma Sh milioni 863
(Tarime), Sh milioni 749 (Msalala) na Sh milioni 843 kwa Halamshauri ya Wilaya
ya Kahama. Changamoto kubwa na namna ambayo fedha hizo zitatumika huko ili
wananchi waone faida ya uwapo wa migodi nadhani hili linapaswa kufuatiliwa
zaidi,
Maoni
Chapisha Maoni