Uhaba wa madarasa: Wanafunzi wasomea chini ya mti
WANAFUNZI wa
Shule ya Msingi Chang’ombe B, iliyopo katika Manispaa ya Dodoma, wanalazimika
kusomea chini ya mti kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.
Taarifa hiyo
ilitolewa mjini Dodoma juzi na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Jacob Kalonga,
alipokuwa akitoa taarifa kwa Ofisa Elimu, Mkoa wa Dodoma, Juma Kaponda,
aliyekuwa ametembelea shuleni hapo
Kalenga
alimwambia ofisa elimu huyo kwamba shule hiyo ina vyumba vitatu vya madarasa na
chumba kimoja cha darasa hakijakamilika kwa kipindi cha miaka minane.
"Shule
yetu ina wanafunzi 761 na idadi halisi ya vyumba vya madarasa
inayohitajika ni vyumba 18 na madawati 254, lakini kwa sasa kuna madawati
60 tu.
“Kwa kuwa
hatuna vyumba vya madarasa vya kutosha, wanafunzi wanalazimika kusomea chini ya
mti mkubwa uliopo shuleni hapa na mti huo hutumiwa na madarasa mawili tofauti.
“Uhaba wa
vyumba vya madarasa na madawati unatokana na mwamko mdogo wa wazazi wa
kuchangia ujenzi wa madarasa pamoja na michango mingine wanayotakiwa kutoa,”
amesema Mwalimu Kalonga.
Diwani wa Kata
hiyo, Bakari Fundikira, amesema tatizo hilo ni kubwa, hivyo akataka viongozi
waliotembelea shuleni hapo washirikiane kulitatua
Maoni
Chapisha Maoni