Waandamana kupinga ubaguzi Afrika Kusini
Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wanaandamana kupinga wimbi la visa vya hivi majuzi vya mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni.
Mikutano
mikubwa imeandaliwa katika mji mkuu Johannesburg na katika mji wa Port
Elizabeth ulioko kusini mwa nchi hiyo ambao ulishuhudia mashambulio
kadhaa dhidi ya wahamiaji wa mataifa ya kigeni mnamo mwaka 2008.
Makundi
ya kiusalama yanafanya misako katika majumba ya makaazi katika mji wa
Alexandra mjini Johannesburg, mahala ambapo mashambulio kadhaa dhidi ya
raia wa kigeni hasa Afrika yalifanyika katika kipindi cha majuma kadhaa
yaliyopita.
Mwaandishi wa BBC anasema kuwa, kuonekana kwa walinda usalama barabarani kumeleta udhibiti na amani.-bbc
Maoni
Chapisha Maoni