Rais Omar al Bashir ashinda uchaguzi
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir amechaguliwa kwa muhula mwengine wa miaka mitano kuendelea kuiongoza nchi hiyo.
Omar al-Bashir ameitawala Sudan kwa zaidi ya miaka 26 sasa.
Ameshinda
uchaguzi wa sasa kwa zaidi ya asilimia 95 kwani wapinzani wake
walisusia
wakisema uchaguzi huo haungekuwa huru na wa haki - kauli
inayoungwa mkono na mataifa ya Ulaya.
Rais Bashir angali anakabiliwa na agizo la kukamatwa na koti ya
kimataifa ICC inayomtuhumu kuhusika katika mauaji ya kimbari huko Dafur.
Baada
ya uchaguzi huu ameahidi kutatua matatizo yanayowakumba raia wa Sudan
ikiwemo matatizo ya kiuchumi na kisiasa
yanayokumba taifa hilo.-bbc
yanayokumba taifa hilo.-bbc
Maoni
Chapisha Maoni