Ratiba ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya
Ratiba ya nusu fainali ya michuano hiyo imepangwa muda mfupi uliopita, huko Nyon – Uswiss.
Ratiba inaonyesha Luis Enrique ataiongoza FC Barcelona kukupiga dhidi
ya FC Bayern Munich inayofundishwa na mchezaji mwenzie wa zamani wa
Barca – Pep Guardiola.
Guardiola na Luis Enrique walikuwa kwenye kikosi kimoja cha Barca kilichokuwa kikifundishwa na Van Gaal msimu wa 1999/2000.
Kwa upande mwingine mabingwa watetezi wa kombe hilo, Real Madrid
watacheza dhidi ya Juventus. Mechi za raundi ya kwanza zitachezwa Mei 5
na 6 na marudiano zitakuwa wiki moja itakayofuatia ya tarehe 12 na 13.
Maoni
Chapisha Maoni