Wanawake 5 kupigania taji la soka la BBC
Mashabiki wanapewa fursa kumpigia kura mchezaji bora wa soka wa BBC
mwaka huu kwa upande wa wanawake likiwa ni taji la kwanza kuandaliwa na
chombo cha habari cha kimataifa.Taji hilo litawasheherekea wachezaji
wenye mchezo wa juu wanaoshindana katika mchezo unaoimarika kwa kasi
duniani.Jopo la wataalam wakiwemo wasimamisi,waandishi,makocha na
wachezaji wa zamani wanashirikiana kumtafuta mcheza huyo miongoni mwa
wachezaji watano walioteuliwa.
Wanaogombania taji hilo watatangazwa mnamo
tarehe 26 mwezi Aprili huku mshindi akitangazwa mnamo mwezi May.''Tuzo
hilo ni fursa muhimu kuangazia viwango vya mchezo na vipaji vilivyopo
katika soka ya wanawake duniani,'' alisema Caroline Rigby,muhariri mkuu
wa taji la BBC la mchezaji bora wa soka ya wanawake mwaka huu duniani.
Taji hilo la BBC lilizinduliwa kabla ya michuano ya kombe la dunia
upande wa wanawake itakayofanyika nchini Canada mwezi Juni.Veronica Boquete (Spain and Frankfurt) Kiungo wa kati
huyo mwenye miaka 27 alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uhispania
iliofuzu katika dimba la kombe la dunia kwa mara ya kwanza.Akiwa mwenye
kipaji cha kufunga mabao amefunga mabao 29 kati ya mechi 42
alizocheza.Pia anajulikana kama mwanamke ambaye mwaka 2013 alianza
kampeni ya kuwashirikisha wachezaji wa kike katika msururu wa mechi za
FIFA za kutoa faraja alipopata sahihi 20,000 .Amesema kuwa :''Ninafurahi
kuteuliwa katika orodha ya taji la mchezaji bora wa soka upande wa
wanawake duniani.Hii inamaanisha kuwa nimekuwa nikifanya kazi nzuri
miaka iliopita.pia inanipa motosha katika siku zijazo''.Marta (Brazil and FC Rosengard) Marta anadaiwa kuwa
maarufu katika soka ya wanawake duniani.akiwa na umri wa miaka
29,mshambuliaji huyo wa kikosi cha Brazil amefunga bao moja katika kila
mechi ya kimataifa aliyocheza akionekana kuwa juu ya kipawa chake.Baada
ya kushinda ligi ya nyumbani mwaka 2014 nchini Sweden kwa mara ya
sita,alishindwa katika fainali ya kilabu bingwa Ulaya upande wa akina
dada-lakini Marta alishinda taji la ligi kuu nchini Sweden Svenska mwaka
huu. Anasema kuwa:''nafurahi sana kwa kuteuliwa.Tayari najihisi mshindi
kwa kuorodheshwa katika fainali ya wachezaji watano.Ni muhimu kwa kuwa
unahukumiwa na mashabiki wa soka,wale wanaokufuata''.
Kim Little (Scotland and Seattle Reign) Mchezaji
Scotland Little amekuwa na msimu mzuri katika ligi ya soka ya wanawake
nchini Marekani ambapo anacheza kama mshambuliaji wa kiungo cha
kati.Scotland aliongoza kwa mabao 16 mbali na kuchaguliwa kama mchezaji
bora wa mwezi mara tatu mbali na kutajwa kuwa mchezaji bora katika msimu
ambao timu yake Seattle,ilifuzu katika fainali kabla ya kupoteza mechi
hiyo kwa kilabu ya Kansas.Ijapokuwa ana miaka 24,amecheza katika
michuano ya kulipwa tangu mwaka 2006 na mwaka 2013 alichaguliwa kama
mchezaji bora wa taji la PFA.Hatahivyo anaendelea kujiliwaza baada ya
Scotland kushindwa kufaula kwa dimba la duniani nchini Canada
2015.Anasema:''Kufuatia kuwepo kwa wachezaji bora duniani na katika ligi
ya Marekani kwangu mimi ni heshima kubwa kutambulika''.
Nadine Kessler (Germany and Wolfsburg)
Ni nahodha wa timu bora barani Ulaya mbali na kuwa tegemeo la timu ya
taifa ya Ujerumani, hakuna taji lolote katika soka ya wanawake ambalo
Kessler hajashinda.Mchezaji huyo wa miaka 27 aliiongoza klabu ya
Ujerumani Wolfsburg kushinda taji lao la pili la ligi ya wanawake barani
Ulaya UEFA pamoja na taji la ligi ya Bundesliga msimu uliopita.Yote
haya yalimwezesha kupata taji la FIFA la mchezaji bora wa mwaka 2015
duniani upande wa akina dada na kumrithi mchezaji mwenza wa Ujerumani
Nadine Angerer.Hatahivyo kuna maswali mengi kuhusu iwapo majeraha mengi
aliyonayo yatamruhusu kung'ara katika dimba la Canada mwaka
huu.Anasema:''nilitaka kucheza soka ili kufanikiwa.lakini sidhani kwamba
kitu kama hiki kinaweza kufanyika''.Asisat Oshoala (Nigeria and Liverpool) Chipukizi Asisat
Oshoala ni mchezaji wa kwanza kutoka Africa kushindana katika ligi ya
soka ya wanawake.Akiwa na mataji ya mchezaji bora wa mwaka na mchezaji
bora chipukizi mwaka huu,alijiunga na mabingwa wa ligi Liverpool kutoka
Rivers Angels.Kwa jina la utani Seedorf,alikuwa mchezaji bora wa mchuano
wa kombe la dunia kwa vijana wasiozidi miaka 20 pamoja na kuisadia
Nigeria kufuzu katika kombe la dunia nchini Canada.Vilevile alituzwa na
rais wa Nigeria .Anasema:''Nahisi kukubalika. Niliweka juhudi kubwa
mwaka uliopita lakini nimeshangazwa na uteuzi huu.Tuzo hii ni kitu
kizuri sana katika soka ya wanawake, inaweza kutusaidia kwa kutoa
motisha kwa mataifa mengine kuwasaidia wanawake wao na kuwachukulia sawa
tu na wanaume''.
Maoni
Chapisha Maoni