Mbaya wa Simba ‘awatishia amani’ Tambwe, Ngassa

MSHAMBULIAJI wa Mgambo Shooting ya Tanga aliyeiua Simba Uwanja wa Mkwakwani jijini humo, Malimi Busungu, amesema kuwa iwapo atafanikiwa kutua Yanga hatamhofia yeyote katika kutekeleza majukumu yake, yaani kucheka na nyavu.
 Inline image 1
Busungu alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliofunga katika mchezo huo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Simba, kwenye ushindi wa mabao 2-0.
Kutokana na umahiri wake wa kucheka na nyavu, kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji waliopo kileleni kwenye orodha ya wafungaji, akiwa na mabao nane.
Akizungumza na BINGWA baada ya mechi yao dhidi ya Simba Uwanja wa Taifa juzi, Busungu alikiri kuwepo kwa mazungumzo baina yake na viongozi wa Yanga na kwamba kila kitu kinakwenda sawa.
Mechi hiyo ya aina yake ilimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, huku Mganda, Emmanuel Okwi akipiga ‘hat’trick’. Bao jingine la Wekundu wa Msimbazi lilitiwa kimiani na Ramadhan Singano ‘Messi’.
Busungu ambaye ni tegemeo ndani ya kikosi cha Mgambo, alisema kuwa akiwa kama mchezaji hawezi kumhofia mchezaji mwenzake, isipokuwa kujituma zaidi ili kuweza kupata nafasi ya kucheza.
“Mazungumzo baina yangu na Yanga yapo lakini bado hayajakamilika na kama yatakuwa sawa na kuweza kujiunga na timu hiyo, basi siwezi kumhofia mshambuliaji yeyote kati ya waliokuwepo hivi sasa kwenye timu hiyo kwani najiamini na kile ninachokifanya,” alisema.
Akizungumzia kupoteza mechi yao dhidi ya Simba, Busungu alisema kipigo walichokipata ni moja ya matokeo ya mchezo, akikiri wapinzani wao kuwazidi maarifa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4