TFF yatembeza adhabu kali Ligi Kuu
MWAMUZI wa mechi kati ya Azam FC na Kagera Sugar,
Stephen Makuka na msaidizi wake namba mbili Said Mnonga wameondolewa kwenye
orodha za waamuzi wa Ligi Kuu na kufungiwa kwa muda wa mwaka mmoja baada ya
kushindwa kumudu mchezo huo.
Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein anapelekwa
kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kutoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutaka
kumpiga mwamuzi msaidizi namba 2, Said Mnonga kwenye mechi namba 158 dhidi ya
Azam FC iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya
38(1) ya Ligi Kuu. Katika mechi hiyo Azam iliibuka na ushindi wa mabao
2-1 ambapo
hata hivyo Kagera walikuwa walilalamikia bao la pili lililofungwa na
Gaudence Mwaikimba kuwa
lilikuwa lakuotea hivyo kuibuka vurugu uwanjani hapo kabla ya kutulizwa na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
lilikuwa lakuotea hivyo kuibuka vurugu uwanjani hapo kabla ya kutulizwa na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).
Kizuguto alisema timu ya Ruvu Shooting imepigwa
faini ya Sh 300,000 kwa kosa la kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo
katika mechi na Kagera Sugar iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Pia Maafande hao wamepigwa faini ya Sh 500,000 kwa
kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo.
Nayo Stand
United imepigwa faini ya Sh 500,000 baada ya mashabiki wake kuwatupia chupa za
maji wachezaji wa akiba wa Polisi Morogoro katika mechi iliyochezwa Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga.
Kizuguto alisema, Meneja wa Polisi Morogoro, Manfred
Luambano alitolewa kwenye benchi la Polisi Morogoro kwa kosa la kutoa lugha za
kashfa kwa mwamuzi msaidizi namba moja Martin Mwalyanje na suala lake
linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho hilo. Alisema, kipa wa
Ndanda SC, Wilbert Mweta amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh 500,000
kwa kumkanyaga na kutaka kumpiga mwamuzi Eric Onoka kwenye mechi na Polisi.
Naye kipa Andrew Ntala wa Kagera Sugar amefungiwa mechi
tatu na kupigwa faini ya Sh 500,000 kwa kuingia kwenye vyumba vya waamuzi na
kuwatolea lugha ya matusi.
Pia kamishna wa mechi hiyo, Bevin Kapufi amefungiwa
mwaka mmoja kwa kutoa taarifa isiyo sahihi.
Naye kamishna wa mechi namba 159 kati ya Mbeya City
na Simba, Joseph Mapunda amepewa onyo kutokana na ripoti yake kuwa na upungufu
huku Wekundu hao wa msimbazi wakilimwa faini ya Sh 300,000 kwa kosa la
kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Mgambo Shooting imepigwa faini ya Sh 100,000 kwa
kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting
iliyochezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.
Maoni
Chapisha Maoni