Mkuu wa shule ataka bweni kupunguza mimba
SHULE ya Sekondari ya Zimanimoto iliyopo Kata ya Ruvuma Manispaa ya
Songea mkoani Ruvuma, inakabiliwa na chanagamoto ya ukosefu wa bweni la
wasichana, jambo ambalo linachangia wanafunzi wa kupata mimba.
Hayo yamelezwa na mkuu wa shule hiyo, Kandidus Kowero, mbele ya meneja wa Benki ya Posta tawi la
Songea ,Joseph Shirima, ambaye ameenda kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya
vizuri mitihani ya kidato cha nne kwa mwaka wa 2014.
Kowero amesema kuwa licha ya shule hiyo ambayo ni ya kata kuonyesha kuwa inauwezo wa kufanya vizuri katika mihani yake lakini bado kumekuwepo na changamoto za ukosefu wa nyumba za walimu pamoja bweni la wasichana.

“Mwaka jana kuna mwanafunzi wa kike amefanya mitihani akiwa
na ujauzito wa miezi nane na akapata alama ya pasi,” amesema.
Amesema kuwa kwa hali kijografia ya mahali ilipojengwa shule hiyo ni sehemu
nzuri ya kusomea lakini inatakiwa kuwa na bweni la wasichana kwa kuwa wanafunzi
waliowengi wanatoka umbali mrefu hivyo baadhi yao hukutana na vishawishi.
Mkuu huyo alifafanua kuwa kwa msimu wa mwaka jana 2014
wanafuzi 46 waliweza kufanya mtihani wa kidato cha nne katika hao wanafunzi
waliofanya vizuri ni wawili.
Kwa
upande wake Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Songea , Joseph Shirima wakati
akiwakabidhi zawadi ya Sh 600, 000 kwa wanafunzi wawili waliopata alama za
ufaulu alisema anatekeleza ahadi ambayo aliwaahidi wanafunzi hao siku ya mahafali.
Shirima amesema kuwa sekondaeri za kata hazitakiwi kubezwa kwa kuwa zinauwezo wa wanafunzi wake kufanya vizuri kama jamii itaungana pamoja kutatua kero ambazo huwa zinajitokeza kwenye shule hizo ikiwemo kama suala la bweni kwa wanafunzi wa kike.

Maoni
Chapisha Maoni