Jeshi la Nigeria lawaokoa wasichanai 293
Jeshi limeiambia BBC kwamba wanawake na watoto hao wa kike
walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia
zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana
hao baada ya kuziharibu kambi hizo.
hao baada ya kuziharibu kambi hizo.
"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu
wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo
walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo
ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake
tisini na tatu."
Kwa sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata
hivyo, jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi
waliotekwa katika mji wa Chibok.
"tuko katika mchakato wa
kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini
kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana
mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok
waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea
kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote. "
bbc
Maoni
Chapisha Maoni