Kimbunga chaleta maafa Muleba
Wawili wafariki, 31 walazwa, 380 hawana makazi WATU wawili wamefariki dunia huku wengine 31 wakilazwa Hospitali ya Mkoa wa Kagera, kutokana na maafa yaliyosababishwa na kile kilichodaiwa kuwa ni kimbunga kilichopita kwa dakika tano katika Kisiwa cha Goziba kilichopo Wilaya ya Muleba ndani ya Ziwa Victoria. Pia katika tukio hilo, jumla ya watu 380 hawana makazi baada ya nyumba zao zaidi ya 78 kuezuliwa kutokana na kimbunga hicho. Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dk. Thomas Rutanchuzibwa, alisema alipokea waathirika wa tukio hilo juzi saa tatu usiku wakiwa na hali mbaya kutokana na majeraha mbalimbali. Dk. Rutanchuzibwa alisema waathirika hao walikuwa wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yaokwa mabati, mbao na matofali ambayo yalitokana na upepo kuezua nyumba zao. Alisema kati ya watu 33 aliowapokea hospitalini hapo, wawili walifariki dunia kutokanana kujeruhiwa vibaya. Dk. Rutanchuzibwa alisema ba...