Chadema yahujumiwa Geita
CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtuhumu Mkuu wa Kituo cha
Polisi Bwanga, Mbachi Ulaga kwa kutumia
viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukihujumu.
Mamalamiko hayo yalitolewa jana
baada ya kukamatwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Igando Kata ya Bwera, Daud Maghobhe
(Chadema).
Inadaiwa Mtendaji wa Kata hiyo, Fikiri Thomas alitoa
taarifa akidai kiongozi huyo anazuia
wananchi kuchangia michango ya ujenzi wa maabara.
Katibu wa Chadema Wilaya ya Chato,
Mange Ludomya, alisema mwenyekiti huyo alikamatwa kijijini hapo muda mfupi baada ya
kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji hicho.
Alisema anashangazwa na
kitendo cha kiongozi wao kukabidhiwa ofisi na kukamatwa wakati hajaanza
majukumu.
Ludonya alisema hatua hiyo ni mwendelezo wa matukio ya
viongozi na wafuasi wa Chadema kukamatwa na kubambikizwa kesi kwa lengo la
kuwafanya wananchi wakichukie chama hicho.
"Inakuwaje aelezwe kuwa anazuia
michango ya wananchi wakati kwanza ofisini hajaingia? Huu ni upuuzi unaolenga kuwavuruga wananchi
na kuwatia hofu kutokana na maslahi ya baadhi ya watu wachache,"alisema.
Mkuu wa Kituo hicho cha Polisi Bwanga alikiri kumkamata mwenyekiti huyo
kwa madai ya kulalamikiwa na mtendaji wa kata hiyo kuwa alimzuia kufanya kazi
yake halali aliyoagizwa na serikali.
Maoni
Chapisha Maoni