Edgar ashinda katika matokeo ya awali ya Zambia
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais nchini Zambia yanaonyesha kuwa mgombea wa chama tawala Edgar Lungu anaendelea kuongoza kwa wingi wa kura. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi nchini humo, |
Edgar Lungu |
Edgar wa chama tawala
cha Patriotic Front 'PF' hadi sasa anaongoza kwa kura nyingi katika
vituo 80 vya kupigia kura, kati ya vituo 150. Irene Mambilima, mmoja wa
wajumbe wa tume ya uchaguzi nchini humo amesema kuwa, hadi jana mgombea
huyo wa chama tawala alikuwa anaongoza kwa kura laki tano na 33,613 huku
Hakainde Hichilema, mgombea wa chama cha upinzani cha UPND akiwa nyuma
ya Edgar kwa kura laki nne na 74 elfu na 76. Hali mbaya ya hewa
ilipelekea baadhi ya vituo vya kupigia kura kuendelea na zoezi hilo hadi
jana Alkhamisi. Uchaguzi mkuu nchini Zambia ulianza siku ya Jumanne.
Baadhi ya watazamaji wa uchaguzi huo wamesema umefanyika katika
mazingira ya amani.
Maoni
Chapisha Maoni