Goran: Mbeya City wangetufunga mengi
KOCHA Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, ameibuka na
kali kwa kusema iwapo wapinzani wao Mbeya City wangekuwa vizuri wangeibuka na
ushindi mnono zaidi ya ule wa mabao 2-1 waliopata kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam juzi.
Goran amejikuta akiyasema hayo mara baada ya kipigo
hicho walichokipata ambacho ni cha pili katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania
Bara, wakiwa wameshinda mbili na sare sita.
Akizungumzia mchezo huo, Goran alisema Mbeya City
walikuwa wazuri zaidi yaokuanzia viungo tofauti na wachezaji wake ambao walionekana
kuishiwa pumzi kipindi cha pili.
“Viungo wa Mbeya City walifanya kazi ya ziada
kutupoteza na hata safu yao ya ulinzi ilikuwa vizuri tofauti na sisi, ndio maana
nasema wangekuwa vizuri wangetufunga mengi kuliko haya,”alisema.
Kocha huyo ambaye tayari ameonyesha kukata tamaa kutokana
na mwenendo wa kikosi chake, amesema hana la kufanya kwa sasa kwenye kikosi
hicho kwa kuwa matumaini yake yamefutika.
“Nikimtoa mtu najua anayeingia anaweza kubadilisha
mpira,lakini unakuta mambo yanakuwa tofauti na ulivyofikiria, sijui hata la
kufanya kwa sasa,”alisema.
Goran amechukua mikoba ya Patrick Phiri
aliyetimuliwa ambapo mpaka sasa ameshinda mechi mbili dhidi ya Ruvu Shooting naNdanda
kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.
Wekundu wa Msimbazi kwa sasa wanashika nafasi ya 11
katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, wakiwa na pointi 13 kutokana na mechi 10.-bingwa
Maoni
Chapisha Maoni