Wasichana wafungiwa chumba kimoja gesti
BAADHI
ya wasichana kutoka jijini Dar es Salaam na Moshi mkoani
Kilimanjaro
wamekutwa wakiwa wamefungiwa katika nyumba moja ya kulala wageni wilayani
Karatu wakisubiri kutafutiwa kazi hotelini.
Hayo
yamebainika leo mchana baada
ya mkazi wa Arusha, Erick Joseph (30)
kunaswa
na polisi kwa tuhuma za mbalimbali
ikiwamo
kuwatapeli watu.
Akizungumza
kwa niaba ya wasichana wenzake, Zulpha Ramadhani na Grace Charles waliokuwa
wamelazwa nyumba moja ya kulala
wageni, Stela Ndemo amesema tangazo la
kutafuta wafanyakazi wa hoteli alilipata akiwa mjini Moshi.
“Nikiwa
Moshi Jumapili Saa 5 usubuhi nilipigiwa
simu na mtu huyo akanihoji na kuniambia nimechaguliwa na ninatakiwa kwenda
Karatu kwa ajili ya kuanza kazi. Nilimwambia sintaweza kwenda siku hiyo kwani
sikuwa nimejiandaa.
“Aliniomba
namba za wazazi nikampa namba ya baba akazungumza naye kisha akamwambia ‘mwanao
amepata kazi anatakiwa kwenda Karatu akiwa na
Sh 40,000 kwa ajili ya kushona sare za kazini’,” amedai Ndemo.
Msichana
huyo alidai baada ya kufika Karatu
alikutana na mtuhumiwa huyo aliyemhoji maswali mengi ambayo yalimfanya
asitambue kama alikuwa akitapeliwa.
“Baada
ya mahojiano alinipeleka nyumba ya kulala wageni nikakutana na wenzangu nao
wanasubiri… jana tulipoona muda aliotuambia atakuja kutuchukua saa 6:30
umepita, tukaamua kumpigia simu lakini akapokea polisi,” alisema Ndemo.
Mtuhumiwa
akijitetea mbele ya polisi alidai
anafanya kazi katika mgahawa maarufu jijini Arusha wa Mc Moodies.
Amedai
kazi hiyo ya kuwatafutia watu kazi huwa anaifanya kwa kujitolea kwa sababu watu wengine humuomba awasaidie kutafuta kazi.
Taarifa za
awali kutoka kwa baadhi ya wakaziwilayani hapa zinadai kwamba mtuhumiwa huyo
amekuwa akishiriki vitendo mbalimbali vikiwamo vya kudanganya kuwatafuatia watu kazi na huchukua fedha zao na wakati mwingine wa
watoto wa kike na kutokomea.
Ofisa mmoja wa polisi wilayani
hapa aliwatahadharisha wananchi kuwa makini hasa wazazi
wa watoto wanaotoka vyuo vya masuala ya hoteli na vingine, kujiepusha na
matangazo ya ajira yanayobandikwa mitaani.
Maoni
Chapisha Maoni