Tabia ya virusi vya Ebola yabadilika
Wanasayansi wanaofuatilia ugonjwa wa
Ebola nchini Guinea wamesema kuwa virusi vya Ebola vimebadilika tangu
kubainika mgonjwa wa kwanza mwezi marchi mwakajana.
Watafiti
kutoka taasisi ya Pasteur mjini Paris ambao wamekuwa wakichunguza
sampuli mbalimbali za damu ili kuweza kutafuta namna ya kukabiliana na
virusi hivyo wamesema virusi hivyo vinajibadili.Kwa sasa wataalam hao wanachunguza pia kama mabadiliko hayo ya virusi-bbc yanaweza kubadili mfumo wa maambukizi ya ugonjwa huo.
Ugonjwa Ebola umewaua watu Zaidi ya 8000 huko Afrika Magharibi.
Maoni
Chapisha Maoni