Kubaka kwamtia mwalimu hatiani
JESHI la Polisi Mkoani Kilimanjaro, linamshikilia mwalimu wa Shule
ya Sekondari Lyakrimu iliyopo Kata ya Mwika, Tarafa ya Vunjo Mashariki, Samson
Lyimo, kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi anayesoma kidato cha tatu (jina
limehifadhiwa).
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Geofrey Kamwela,
amesema tukio hilo lilitokea
Januari 28, mwaka huu.
Alisema kumbukumbu zinaonyesha mwalimu huyo ana rekodi ya
matukio ya ubakaji.
Kamanda Kamwela, amedai kuwa mwanafunzi huyo mwenye umri wa
miaka 16, alibakwa na mwalimu wake baada ya kumuita kwenye chumba cha maabara
na kuanza kumtomasa, akamvua nguo kwa nguvu na kumbaka, hivyo kumsababishia
maumivu makali.
Hata hivyo, baada ya mtuhumiwa kufanya kosa hilo, anadaiwa
alijaribu kutoroka hadi alipokamatwa na polisi eneo la Himo.
Mmoja wa walimu ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini,
aliliambia MTANZANIA kuwa mwalimu huyo anadaiwa kufanya matukio ya ubakaji wa
wanafunzi pamoja na kuwapa ujauzito kwenye shule zaidi ya mbili wilayani Rombo.
Maoni
Chapisha Maoni