Diwani alalamikia harufi za maiti kituo cha afya
DIWANI wa Kata ya Bulungwa mkoani
Shnyanga, Joseph Masaluta, ameilalamikia Halmashauri ya Wilaya ya
Ushetu kwa kujenga kituo cha afya katika kata hiyo
bila kuwapo chumba cha kuhifadhia maiti.
Alisema ndani ya kituo hicho
kumekuwapo harufi kali kutokana na wagonjwa wanaofariki dunia
kutunzwa kwenye vitanda wanakolazwa.
Malalamiko hayo aliyatoa juzi kwenye kikao cha baraza la madiwani cha halmshauri ya Ushetu kilichokuwa kikipitia bajeti na mpango wa maendeleo wa halmashauri hiyo.
Malalamiko hayo aliyatoa juzi kwenye kikao cha baraza la madiwani cha halmshauri ya Ushetu kilichokuwa kikipitia bajeti na mpango wa maendeleo wa halmashauri hiyo.
Alisema kutokuwapo sehemu
ya kufidahia maiti katika kituo imekuwa ni kero kwa wananchi wa kata hiyo.
“Huwezi kujua marehemu ni nani na
aliyelazwa ni nani kwa kuwa vitanda vimeongozana hali ambayo hata mtu akifa na
ndugu yake kuchelewa kuchukua mwili
inakuwa ni shida kwa wale walio jirani.
Tumechoka na harufi katika kituo hicho.
“Tunaiomba Halmashauri ya Ushetu
kuhakikisha inajenga chumba cha kuhifadhi maiti wananchi waepuke adha wanapokwenda kupata
huduma,” alisema.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu,
Isabela Chilumba, alisema
halmashauri inatarajia
kutenga fedha kwa ajili ujenzi wa chumba hicho.-Mtanzania
Maoni
Chapisha Maoni