…Tambwe ni habari nyingine Yanga
MSHAMBULIAJI
wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe, ameonekana kulimaliza tatizo la ukosaji mabaokutokana
na kufanya kweli kwenye mazoezi ya timu hiyo mjini Bagamoyo.
Kikosi
cha Yanga kinachonolewa na Mholanzi, Hans van der Pluijm, kimehamishia kambi
katika Chuo cha Uvuvi Mbegani, Bagamoyo kujiwinda na michezo yake kadhaa ya
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga
itashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam keshokutwa (Jumapili)kuwavaa Ndanda FC
ya Mtwara kwenye mfululizo wa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwenye
mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wachuo hicho cha uvuvi, Tambwe
ameonyesha kuwa na uchu wa kuzifumania nyavu baada kuonekana kuiva na kuzifuata
vyema mbinu za Pluijm.
Siku
za karibuni safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ikiongozwa na Kpha Sherman,Danny
Mrwanda,Tegete na Hussein Javu,imekosa umakini na kusababisha washambuliaji hao
kukosa mabao ya wazi kwenye michezo kadhaa ya Ligi Kuu iliyokwishacheza.
Kutokana
na hilo kocha Pluijm na wasaidizi wake, Charles Boniface Mkwasana Juma
Pondamali muda wote wameonekana kulifungia kazi zoezi la ufungaji wakiwa
mazoezini.
Pluijm ameonekana kuwapa mbinu mpya vijana wake kwakuwafundisha
namna ya kupachika mabao,huku Tambwe akionekana kuwa kinara zaidi wa kuzielewa
mbinu zake.
Pluijm kama kawaida yake aliwataka washambuliaji
wake; Tambwe,Sherman,Hussein Javuna Tegete,kufunga mipira itakayotokana na krosi
kutoka upande wa kulia na kushoto mwa uwanja kuwafunga makipa Deogratius Munishi‘Dida’
na Ally Mustapha ‘Barthez’.
Katika zoezihilo la upigaji krosi lililodumu kwa takribani
dakika 30,Tambwe alionekana kinara zaidi wa kuunganisha krosi na kufunga mabao manne
kutokana na mashuti makali ya mguu wakulia kumtungua kipa Barthez.
Tambwe alifunga mabao hayo kutokana nakrosi kutoka
kwa winga, Simon Msuvana beki wa kushoto, Charles Edward ambao walipewa jukumu
la kupiga krosi hizo.
Wakati Tambwe akifanya yake, wenzake Sherman,Tegete,
Javu nao hawakuwa nyuma kwenye zoezi la kufunga kutokana namashuti nje ya 18.
Kwenye zoezi hilo, washambuliaji hao kila mmoja
alifanya vyema zoezi hilo ambapo Sherman, Tegete na Javu kila mmoja alifunga mabao
mawili, huku Mrwanda na Javu wakiambulia bao moja kutokana na mashuti matano.
Yanga imeendelea na mazoezi yake jana kwenye Uwanja
wa Chuo cha Uvuvi Mbegani kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara
dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara utakaopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.-Bingwa
Maoni
Chapisha Maoni