Kinara wa mirungi atiwa hatiani

MTU anayedaiwa kuwa msafirishaji maarufu wa mirungi kwa nchi za Afrika Mashariki, Joram Mwakalalebela (48), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Wilaya ya Mbozi kwa tuhuma za kukutwa na mirungi kilo 80.http://lisatorracolaw.com/wp-content/uploads/2013/03/LisaTorracoSlider.jpg
 Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, Rahimu Mushi, mwendesha Mashtaka wa Polisi, Inspekta Samweli Sarro, alisema mshtakiwa alifanya kosa hilo Januari 24, mwaka huu.
Alisema mshtakiwa alikutwa katika nyumba ya kulala wageni ya Jabari iliyopo Sogea mjini Tunduma saa 3:30 asubuhi, akiwa na dawa za kulevya aina mirungi kilogram 80.
Hata hivyo, mshtakiwa alikana kosa hilo na kesi kuahirishwa hadi Februari 10, mwaka huu.-Mtanzania

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4