Kimbunga chaleta maafa Muleba
Wawili wafariki, 31 walazwa, 380 hawana makazi
WATU wawili wamefariki dunia huku wengine 31
wakilazwa Hospitali ya Mkoa wa Kagera, kutokana na maafa yaliyosababishwa na
kile kilichodaiwa kuwa ni kimbunga kilichopita kwa dakika tano katika Kisiwa
cha Goziba kilichopo Wilaya ya Muleba ndani ya Ziwa Victoria.
Pia katika tukio hilo, jumla ya watu 380 hawana makazi
baada ya nyumba zao zaidi ya 78 kuezuliwa kutokana na kimbunga hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo,
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dk. Thomas Rutanchuzibwa, alisema alipokea
waathirika wa tukio hilo juzi saa tatu usiku wakiwa na hali mbaya kutokana
na majeraha mbalimbali.
Dk. Rutanchuzibwa alisema waathirika hao walikuwa
wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yaokwa mabati, mbao na matofali ambayo
yalitokana na upepo kuezua nyumba zao.
Alisema kati ya watu 33 aliowapokea hospitalini
hapo, wawili walifariki dunia kutokanana kujeruhiwa vibaya.
Dk. Rutanchuzibwa alisema baadaya kupokea taarifa ya
tukio hilo, aliunda tume haraka na kwenda eneo la tukio kwa kutumia boti ili
kuokoa na kutoa huduma ya awali huku madaktari wengine wakibaki hospitalini kwa
lengo la kutoa huduma.
“Boti zilizoleta wagonjwa hao zilikuwa tatu, moja ilifika
hapa saa tatu na nyingine ilifikia saa tisa usiku zikiwa na idadi ya waathirika
31, kati ya hao wanawake walikuwa 14, wanaume 17 huku waliokuwa wamekwisha
fariki walikuwa wawili.
“Kwa ujumla wagonjwa hao 31 tuliowapokea wanaendelea
vizuri isipokuwa watatu ambao tumewafanyia uchunguzi kwa kuwapiga picha za X-ray
ambapo wanaume wawili wamegundulika kuvunjika mifupa na mwanamke mmoja
amegundulika kuwa na maumivu makali kichwani.
Dk. Rutanchuzibwa alisema waliofariki hadi sasa
hawajatambuliwa majina yao na kuwataka ndugu kufika hapo kwa ajili ya utambuzi.
Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Lembris Kipuyo,
amelazimika kwenda eneo la tukio kwa lengo la kujionea hali ilivyo.
Akizungumzana gazeti hili kwa njia ya simu akiwa
eneo la tukio, alisema baada ya kupata taarifa alilazimika kwenda huko akiwa na
baadhi ya dawa ambapo aliwapata watu 40 waliojeruhiwa na kwamba madaktari
waliokuwapo waliendelea kuwapa huduma.
“Hapa halini mbaya kwani watu wengi wamejeruhiwa na
baadhi ya makazi yao yameezuliwa na upepo huo, kwa takwimu nilizopewa ni kwamba
nyumba 78 ambazo kati ya watu 380 waliokuwa wanaishi, zimebomolewa hivyo watu
hao hawana pa kuishi.
“Tayari kamati ya maafaya wilaya pamoja na wataalamu
wengine wamefika hapa Goziba kwa lengo la kutoa huduma kwa waathirika, hivyo
ninawaomba wananchi kuwa watulivu kwani Serikali inashughulikia tatizo
hili,”alisema.
Kipuyo alisema mbali ya makazi ya watu huharibiwa,
pia kimbunga hicho kiliharibu zahanati ya Goziba iliyojengwa na Kampuni ya simu ya Vodacom
pamoja na kituo cha polisi kwa kuezuliwa mabati.
Alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia tukio hilo,
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella na Kamanda wa Polisi mkoa huo, Henry
Mwaibambe, hawakupatikana.-Mtanzania
Maoni
Chapisha Maoni