Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2014

Man U yaambulia patupu EPL

Picha
Nahodha wa kikosi cha Man U wayne rooney baada ya timu hiyo kupata sare ya 0-0 dhidi ya Totenham Harakati za Manchester United kujaribu kuwafikia Chelsea na mabingwa wa ligi hiyo Mancity zilipata pigo baada ya kupata sare ya 0-0 dhidi ya Totenham Hotspurs. United ilitengeza nafasi nyingi za wazi katika kipindi cha kwanza huku shambulizi la Juan Mata likipiga chuma cha goli. Hatahivyo mlinda lango wa Totenham Hugo Lloris alilazimika kufanya kazi ya ziada baada ya kuwanyima mabao Radamel Falcao,Robin Van Persie na Ashley Young. Kiungo wa kati wa Spurs Andros Townsend alifanya mashambulizi makali katika ngome ya manchester United huku Ryan Mason akikosa bao la wazi katika dakika za mwisho. Kikosi hicho cha Mauriccio Pochettino kimekuwa kikifunga mabao yake katika dakika za lala salama dhidi ya Swansea na Leicester lakini licha ya kudhibiti mpira dakika 15 za mwisho katika kipindi cha pili hawakuweza kupata bao

Taarifa mpya: Indonesia yasitisha utafutaji wa Airasia

Picha
Indonesia imesitisha utafutaji wa ndege ya AirAsia hadi kesho iliopotea na takriban abiria 160 waliokuwa wakielekea Singapore kutoka mji wa Surabaya nchini Indonesia. Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka. Ndugu na familia za waathiriwa wa AirAsia wakisubiri habari za kutweka kwa ndege hiyo Takriban abiria 162 walikuwa wakiabiri ndege hiyo aina ya Airbus 320 wengi wao wakiwa raia wa Indonesia. Airasia iliotoweka Rubani wa chombo hicho anadaiwa kutaka kubadilisha njia ili kuepuka kimbunga lakini hakuomba usaidizi wowote. Baadhi ya meli katika eneo hilo zinaendelea kuitafuta ndege hiyo,licha ya hali mbaya ya hali ya anga Familia na marafiki wa waathiriwa wamekongamana nchini Singapore na uwanje wa ndege wa surabaya wakingojea habari kuhusu ndege hiyo.-bbc

Hadith: Mwalimu Magdalena sehemu ya 6

Picha
Ilipoishia wiki iliyopita MWALIMU mpya kijijini hapo, Mwalimu Jokam (Joka) amefika kwa mwenyekiti bila kujulikana kama ndiye aliyemsaidia Mwalimu Magdalena asipate madhara kwa mwenyekiti wa kijiji hicho. Mwalimu Magdalena naye anajikuta akiwa katika wakati mgumu kwani baada ya kupitiwa na usingizi alipokuwa na mwanafunzi John, mgeni wake aliyekuwa amemficha chini ya uvungu wa kitanda chake alishindwa kuvumilia akaamua kuondoka na leo kwa mara ya kwanza wanakutana wakiwa darasani,  Sasa endelea kufuatilia hadithi hii ya kusisimua ya Mwalimu Magdalena. Katika hali isiyotarajiwa wakati mwalimu Magdalena akimaliza kipindi chake cha historia kipindi kilichofuata ni hisabati, kilichofuata hapo ni hali ya mshangao uliotoka kwa mwalimu Magdalena. Kitendo cha mwalimu Magdalena kumuangalia kwa muda mrefu mwalimu Joka kilitafsiriwa tofauti na John, lakini hakikuleta fikra tofauti kwa kuwa imani ya wanafunzi ni kwamba walimu hao ndiyo kwanza walikutana. Haikuwezekana kunyamaza k

Umeisikia hii ya Bomu kumuua aliyetaka kuua polisi Songea

Picha
MTU mmoja amefariki dunia papo hapo baada ya bomu alilotaka kuwarushia askari waliokuwa doria ya Sikukuu ya Krismasi katika Mtaa wa Kotazi uliopo Kata ya Majengo, Manispaa ya Songea, kumlipukia. Kutokana na tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia jana, Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na makachero kutoka makao makuu ya jeshi hilo yaliyopo Dar es Salaam, wanawasaka watu watatu walioshirikiana na mlipuaji huyo ambaye bomu hilo lilimshinda na kumlipukia huku utumbo wake ukitoka nje na mkono wake wa   kushoto umekatika na vipande vyake havijulikani vilipo. Akizungumza mjini hapa jana katika ukumbi wa mikutano wa jeshi hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athumani, alisema tukio hilo lilitokea saa saba usiku wakati askari wakiwa doria. Alisema wakati doria inaendelea katika eneo hilo, kulitokea mlipuko wa bomu lililotengenezwa kienyeji na kuwajeruhi askari wawili. Aliwataja askari waliojeruhiwa kuwa ni PC Mselemu mwenye namba G 7903, am

Mgombea wa Chadema, kampeni meneja wauawa

Picha
ALIYEKUWA mgombea nafasi ya uenyekiti wa Kitongoji cha Idodomya Kata ya Kanoge Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, Williamu Masanilo (Chadema) na mpambe wake Juma Ujege, wameuawa kwa kukatwa kichwa. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda alisema tukio hilo ni sawa na matukio mengine ya ujambazi na kukanusha taarifa zilizodaiwa kuwa lina uhusiano na masuala ya kisiasa. Alisema tukio hilo limetokea Desemba 24 mwaka huu saa 8 usiku ambapo watu wasiojulikana walivamia nyumbani kwa William Masanilo ambaye ni mfanyabiashara na kufanikiwa kumchoma na kitu chenye ncha kali  kichwani na hivyo kumsababishia kifo chake. “Wavamiaji hao walitaka fedha, baada ya kumuua walimgeukia mfanyakazi wake ambaye walitaka atoe fedha lakini alipowajibu hajui walimpiga na kitu kizito kilichosababisha kupasuka kichwani na hivyo kufariki, uchunguzi wetu awali wa unaonyesha hili tukio ni la ujambazi na si la siasa,” alisema kamanda. Katibu wa Chadema Wilaya ya Kaliua, Rajabu Hamisi yeye a

Mbaroni kwa kukutwa na meno ya tembo

Picha
JESHI la Mkoa wa Katavi linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo vipande 22 vya uzito wa kilogramu 46 yenye thamani ya Sh milioni 157.5. Imeelezwa kutokana na uzito huo, imebainika ni sawa na tembo saba  waliouawa wakati wakiwa wanataka  kuyasafirisha kwenye basi kutoka Mpanda kuelekea mkoani Kigoma. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi, Rashid Mohamed, aliwataja watuhumiwa hao  waliokamatwa kuwa ni Justine Baluti (Zolros) (39) mkazi wa Kijiji cha  Ivungwe makazi ya wakimbizi ya Katumba Wilaya ya Mlele na  Bobifaphace Hoza (40) mkazi wa Kalele  Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma. Alisema watuhumiwa hao wote wawili walikamatwa jana saa 12 wakiwa katika harakati za kusafirisha meno hayo katika Stendi ya mabasi ya Mpanda. “Siku hiyo ya tukio majira hayo ya saa kumi 12 asubuhi, askari polisi walikuwa doria kwenye eneo la stendi ya mabasi ya Mpanda yaendayo mikoani, walimtilia shaka mtuhumiwa Justine Baluti  aliyekuwa anapakia mizigo

Jaribio la kuiba sanamu la Bikira Maria lakwama

Picha
VIJANA wa tatu wakazi wa Mtaa wa Luwawasi, Manispaa ya Songea,   wametakiwa kwenda na wazazi wao kutubu dhambi  za kutaka kuiba mapambo ya kanisa pamoja na sanamu ya Bikira Maria katika Kanisa Katoliki la Kigango cha Samora. Mapambo hayo pamoja na sanamu inayomuonesha mtoto Yesu vilipambwa kwa ajili ya sherehe za Krismasi. Akizungumzia tukio hilo katika ibada ya Sikuku ya Krismasi iliyoongozwa na Padri Cristom Kapinga na Katekista wa kigango hicho, Keneth Mhagama walisema vijana hao walifanya jaribio hilo usiku wa manane baada ya ibada ya mkesha kumalizika. Mhagama alisema kuwa kilichosaidia washindwe kufanya uharifu ndani ya kanisa hilo ni kutokana na kigango hicho kuweka walinzi ambao walifanikiwa kuwadhibiti wahalifu hao ambapo baada ya kuwatia mbaroni katika maelezo yao walijitambulisha majina yao na eneo wanaloishi kuwa ni Mtaa wa Luwawasi. “Tunawataka hao vijana waje kutubu dhambi zao pamoja na na wazazi wao ili tuweze kumaliza suala hili kiroho na hata kuwanja kat

Polisi wapokea msaada wa kompyuta

Picha
ASKOFU wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime, Dk. Mwita Akiri, ametoa msaada wa kompyuta pamoja na mashine ya kudurufu kwa Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Polisi la jinsia kwa ajili ya kusaidia utunzaji wa takwimu na ukatili na kuratibu masuala mbalimbali. ASKOFU wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime, Dk. Mwita Akiri Akikabidhi msaada huo wenye thamani ya Sh milioni 1.2, Askofu Akiri alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya kuimarisha jitihada za jeshi hilo katika kukomesha vitendo vya ukeketaji watoto wa kike unaoendelea wilayani Tarime. Alisema kama viongozi wa kanisa wanaamini kuwa mila ya kukeketa huathiri afya na maumbile ya watoto wa kike ambao ni watoto wa Mungu na inapaswa kukomeshwa hivyo kuwashauri wazee wa mila kusaidia kuzuia mila hiyo. Makabidhiano hayo yamefanyika jana Kituo cha Polisi wilayani Tarime na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wilaya ya Tarime, Issa Bukuku mbele ya Kaimu Mkuu wa Wilaya, Jonathan Machango pamoja na K

Mwanamke achoma moto nyumba ya mumewe

Picha
MKAZI wa Kijiji cha Majengo, Kata ya Koryo Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara, Vaileth Ogola, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kuchoma nyumba ya mumewe moto na kuteketeza mali zilizokuwamo. Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Tarime na Rorya, Lazaro Mambosasa, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 23 mwaka huu saa mbili usiku mara baada ya kutokea ugomvi baina yake na mumewe. “Tukio hili linadaiwa kuwa chanzo chake ni ugomvi uliosabaishwa na wivu wa kimapenzi baina ya mtuhumiwa na mumewe, Kinyatta Kibindi, lakini baada ya kufanikiwa kuichoma moto nyumba hiyo alitoroka na kwenda ambako hakujajulikana na hivyo Jeshi la Polisi linamsaka,” alisema. Hata hivyo, Kamanda alisema kuwa mumewe Kibindi ni mkazi wa Dar es Salaam na alikuwa ameenda kijijini hapo kwa nia ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya lakini sasa hana makazi ya kuishi yeye pamoja na wapangaji saba waliokuwa wakiishi katika nyumba hiyo.

Obama:Filamu ya Kim Jong Un ionyeshwe

Picha
Rais wa marekani Barack Obama ameimbia Korea Kaskazini kuwa Marekani itajibu kisa ambapo wizi wa mtandao ulioendeshwa dhidi kampuni ya filamu ya Sony Pictures hali iliyosababisha kufutiliwa mbali kwa maonyesho ya filamu inayomdhihaki kiongozi wa korea kaskazini kim jong- un. Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa hatua hiyo haitakuwa rahisi kwa Marekani kutokana na kujitenga kwa Korea kaskazini. Filamu ya Kumdhihaki rais wa Korea kazkazini Kim Jong Un iliozuiliwa na kampuni ya Sony Pictures kufuatia vitisho  Obama Rais Obama amesema kuwa kampnui ya filamu ya Sony Pictures ilifanya makosa kwa kusitisha kuonyesha filamu hiyo. Hata hivyo Sony ilisema kuwa ilichukua uamuzi huo kwa kuwa kumbi nyingi kubwa za sinema nchini Marekani zilikataa kuonyesha filamu hiyo. Sony imesema kuwa ina mipango wa kuionyesha filamu hiyo na kwa sasa inatafuta njia zingine za kuionyesha.-BBC

Wauaji wa Ubungo wahukumiwa kunyongwa, Ni wale waliohusishwa na uporaji wa fedha za NMB

Picha
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa hukumu ya   kunyongwa hadi kufa kwa washtakiwa sita  katika kesi ya mauaji ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wa mkoani Morogoro na mfanyakazi wa Benki ya NMB, maarufu kama mauaji ya Ubungo Mataa. Washtakiwa hao waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa jana na Jaji Projest Rugazia ni Haji Kiweru, Mashaka Pastory, Wycliff Imbora, John Mndasha, Martine Mndasha  na Rashidi Abdikadir.   Jaji Rugazia alidai kwamba aliwatia hatiani washtakiwa hao na kuwahukumu kunyongwa hadi kufa kutokana na ushahidi ulitolewa na mashahidi 29 upande wa mashtaka pamoja na vielelezo 78 vilivyowasilishwa mahakamani hapo na ushahidi wa utetezi. “Maungamo ya washtakiwa, ushahidi wa kitaalam na utambuzi wa washtakiwa kutambiliwa eneo la tukio inaonesha wazi kwamba walikuwa na nia ya kujaribu kupora takribani Sh milioni 150 ambazo ni mali ya benki ya NMB zilizokuwa zikisafirishwa kutoka  Dar es Salaam kwenda  Morogoro tawi la Wami,” Alidai Jaji Rug

Binti achinjwa na kunyofolewa sehemu za siri

Picha
MKAZI wa Kijiji cha Ilalangulu, Kata ya Kibaoni wilayani Mlele, Elizabeth Richard (16), amechinjwa na kukatwa titi lake la kushoto na mikono yake kisha akanyofolewa sehemu zake za siri. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari Akzungumza mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema mauaji hayo yalitokea juzi saa nane mchana kijijini hapo. Alisema siku ya tukio binti huyo akiwa na  mumewe aitwaye Hevinie Kagembe  waliondoka nyumbani kwao asubuhi kwenda shamba katika maeneo ya Kazaroho. Ilipofikia saa kumi jioni, Kagambe, alirudi nyumbani kwake lakini hakumkuta mkewe  kama ilivyo kawaida yao licha ya kutangulia kurudi nyumbani kwa ajili ya kuandaa chakula. Alisema ilipofika saa mbili usiku Kagambe alipata shaka kuona hadi wakati huo mkewe hajarudi nyumbani wakati si kawaida yake. “Baada ya kuona hivyo alimpigia simu mkwewe aliyekuwa akiishi kijijini hapo  ili kutaka kujua kama mkewe yuko kwake lakini

Draw ya nne ya Tutoke na Serengeti promotion

Picha
Meneja bia chapa ya Serengeti Premium Lager, Bw.Rugambo Rodney akibonyeza kitufe wakati wa kuchezesha droo ya nne kutafuta mshindi wa tatu wa Limo Bajaj katilka shindano la Tutoke na Serengeti ambapo Isaack Edward Amaro ameibuka mshindi. Katikati ni msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw.Mrisho  Milao na kulia ni mhasibu wa kampuni ya Serengeti (SBL) Monica Labre.hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Meneja bia chapa ya Serengeti Premium Lager, Rodney Rugambo akibonyeza kitufe wakati wa kuchezesha droo ya nne kutafuta mshindi wa tatu wa Limo Bajaj katilka shindano la Tutoke na Serengeti (kulia) ni msimamizi toka michezo ya kubahatisha, Mrisho  Milao .

UZINDUZI WA CHUPA NDOGO YA TUSKER

Picha
Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti wakisikiliza jambo wakati wa uzinduzi wa Chupa mpya ya Tusker yenye mililita 330, katika halfa iliyofanyika leo katika ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Masoko wa kampuni ya bia Serengeti, Bw.Ephraim Mafuru , akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa chupa mpya ya bia ya Tusker yenye ujazo wa milimita 330, hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.  Wahudumu wa kampuni ya bia ya Serengeti wakionyesha mwonekano wa chupa mpya ya bia ya Tusker yenye ujazo wa ml 330 . Kikundi cha sanaa cha Dar es Salaam Dance international(DDI) kikifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa chupa mpya ya bia ya Tusker. Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti wakiwaonyesha waaandishi wa habari , hawapo pichani, mwonekano mpya ya Bia ya Tusker yenye ujazo wa mlimita 330. Meneja masoko-Familia ya bia ya Tusker na Pilsner kampuni ya bia ya Serengeti, Anitha Msangi akiongea na waandishi wa habari , mara baad

Azam FC yatimuliwa Uganda

Picha
SHIRIKISHO la Soka la Uganda (FUFA), limeizuia klabu ya Azam FC kucheza mechi za kirafiki nchini humo kutokana na kutokuwa na taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Azam ipo ziarani Uganda kwa ajili ya kambi ya wiki mbili ikilenga kucheza mechi za kirafiki za kujipima nguvu dhidi ya timu mbalimbali za nchi hiyo. Tayari kikosi cha Wanalambalamba hao kimecheza mchezo mmoja wa kirafiki kati ya minne iliyopanga kucheza dhidi ya SC Villa ambapo ilidunguliwa mabao 3-2. Pia ilipangwa kujipima dhidi ya timu za KCCA FC, Viper na URA kabla ya kurejea nchini kuendelea na Ligi Kuu. Msemaji wa FUFA, Ahmed Hussein alisema: “Hatujapata taarifa yoyote kutoka TFF kama kutakuwa na mechi zozote za Azam, hivyo tumeamua kuizuia hadi hapo watakapotutaarifu,” alisema Hussein. Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa alipoulizwa kuhusiana na taarifa hiyo ya FUFA alikana kuwa na taarifa za safari ya Azam kwenda Uganda.   “Utaratibu ni kwamba timu yoyote inapokwenda kuweka kam

Mke amrudisha Okwi Uganda

Picha
BAADA ya kuiwezesha Simba kuitungua Yanga mabao 2-0 katika pambano la Nani Mtani Jembe, straika Emmanuel Okwi leo Jumanne anaondoka nchini kwenda Uganda kwaajili ya kusherehekea harusi yake. Okwi alifunga ndoa ya kimila hivi karibuni akiwa mapumzikoni nchini kwao Uganda, hatua iliyopelekea kuchelewa kujiunga na kikosi cha Simba kilichokuwa kinajiandaa na mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Yanga. Straika huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichoibuka na ushindi dhidi ya Yanga katika pambano la Nani Mtani Jembe lililopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mabao ya Simba katika mchezo huo yalizamishwa wavuni na Awadh Juma na Elias Maguli. Akizungumza jana, Okwi alisema baada ya sherehe ya harusi iliyohusisha upande wa ndugu zake, leo anarejea nchini kwake katika tafrija nyingine itakayofanyika upande wa laazizi wake. “Unajua ndoa niliyofunga hivi karibuni ilihusisha upande wa familia yetu kwa hiyo narudi Uganda kwaajili ya sh

Wachezaji Simba wajazwa mamilioni

Picha
BAADA ya kuilaza Yanga mabao 2-0 kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe, uongozi wa Simba umewapa wachezaji wao motisha ya fedha kama shukrani kwa kufanikiwa ushindi huo. Simba ilizawadiwa zaidi ya Sh milioni 90 na waratibu wa pambano hilo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kufuatia ushindi huo. Kiasi hicho cha fedha ilichopata Simba  kinajumuisha Sh milioni 15 kwa kuibuka mshindi wa pambano hilo na Sh milioni 77 za kura za mashabiki. Mpinzani wake Yanga alizawadiwa jumla ya Sh milioni 7, kati ya hizo Sh milioni 5 ni kifuta jasho baada ya kupoteza mchezo huo na Sh milioni 2 za kura za mashabiki. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kilisema kuwa wachezaji wote wa timu hiyo wamevuna fedha kufuatia ushindi dhidi ya Yanga. “Wachezaji waliocheza kila mmoja amepewa Sh milioni mbili, wakati wale waliovaa jezi lakini hawakucheza kila mtu ameondoka na Sh milioni moja. “Kuna wale ambao hawakucheza kabisa wala kuvaa jezi, hawa kila mmoja amepata Sh 600,000 kama m

Soka lamfikisha polisi

Picha
Mchezaji na shabiki sugu wa soka mwanamke nchini Saudi Arabia, amejipata mashakani baada ya kuingia katika uwanja uliokuwa na mashabiki wanaume. Viwanja vya soka nchini humo vina masharti yake , kwani wanawake na wanaume hawaruhusiwi kuchanganyikana. Kulingana na taarifa za vyombo vya habari, shabiki huyo mwanamke aliingia uwanjani akiwa amevalia kama mwanamume. Aliingia uwanjani akiwa amevalia kofia kubwa iliyokuwa imefungwa na kitambaa cheusi cha kujitanda kichwani pamoja na mavazi meupe ya timu iliyokuwa inacheza ugenini. Alikaa mbali na mashabiki wengine wanaume akiwa peke yake kazingirwa tu na viti. Lakini hapo ndipo unga ulizidi maji kwani aliweza kutambuliwa Polisi walimkamata na kusema kuwa watampeleka kwa maafisa wakuu. Lakini raha aliyoipata shabiki huyo sugu licha ya masaibu yake ni kwamba klabu aliyokuwa anashabikia iliibuka na ushindi.

Kijana aliyeua watu 42 nchini Brazi

Picha
Sailson Jose das Gracas akiwa chini ya aulinzi Polisi nchini Brazil wamemkamata mwanaume aliyekiri kuwaua watu 42 katika kipindi cha miaka kumi mjini Rio de Janeiro. Polisi wanasema walimkamata Sailson Jose das Gracas mnamo siku ya Jumatano, baada ya kumdunga kisu mwanamke ambaye alifariki muda mfupi baadaye. Alikiri kuwaua wanawake wengine 37 , wanaume watatu na mtoto mdogo wa miaka 2. Polisi wanasema wanawasaka waathiriwa na kusema wameweza kuwapata watu wanne. Katika mahojiano na vyombo vya habari, polisi walisema kua mwanamume huyo kawaida alikuwa anaondoka kwake na kuwawatufuta waathiriwa lengo lake likiwa ni kuua 'kwa raha zake.' Aliambia polisi kuwa wakati atakapoondoka gerezani hatasita kuua tena. Alisema kuwa alipendelea kuwaua wanawake wazungu ambao aliwanyonga. Wanaume watatu ambao aliwaua, alifanya hivyo alipokodiwa kama mamluki. Das Gracas alisema: " Ningesubiri kupata fursa tu kisha ningeingia ndani ya nyumba na kutekeleza mauaji,''

Rais wa Nigeria ampendekeza makamu wake kuwa mgombea mwenza

Picha
Rais Jonathan amemtaja mgombea mwenza baada ya kukubali uteuzi kuwa mgombea pekee wa urais kutoka chama tawala nchini Nigeria, PDP, katika mkutano maalum wa chama uliofanyika jana jioni mjini Abuja.   Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ametangaza kuwa, anampendekeza makamu wake Namadi Sambo kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Februari mwaka ujao. Awali, kulikuwa na tetesi kuwa rais Jonathan angeteua mgombea mwenza mwingine. Sambo alishika madaraka ya makamu wa rais mwaka 2010, na baadaye kuchaguliwa na rais Jonathan kuwa mgombea mwenza kwenye uchaguzi wa mwaka 2011.

Maporomoko yatokea Indonesia, wengi wahofiwa kufa

Picha
Maporo moko ya udongo yametokea katika mkoa wa Java nchini Indonesia na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa. Janga hilo la kimaumbile limetokea usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha. Habari zinasema kuwa miili ya watu wanane imepatikana lakini kuna hofu kwamba waliopoteza maisha ni wengi sana kwani hadi sasa zaidi ya watu 100 hawajulikani waliko. Duru za habari zinasema zoezi la uokoaji linaendelea ambapo polisi, jeshi pamoja na raia wa kawaida wanasaidiana kufukua udongo uliofunika kijiji kizima cha Jemblung. Msemaji wa taasisi ya taifa ya kukabiliana na majanga, Sutopo Purwo Nugroho, amesema, barabara za kuelekea hospitalini pia zimeharibiwa kabisa na mvua zinazonyesha. Mamia ya watu katika maeneo mengine ya mkoa huo wa Java wameondolewa na kupelekwa katika maeneo salama.

Uliziona hizi picha za hawa waandamanaji

Picha
Haya ni Maandamano ya nchi nzima katika kulalamika dhidi ya mauaji yanayofanywa na polisi huko Missouri na New York ambayo yaliendelea wiki nzima. - Dec. 9, 2014

Marekani yaidhinisha matumizi makubwa kwa ajili ya ulinzi

Picha
Baraza la seneti la Marekani limeidhinisha zaidi ya dola nusu trilioni kwa matumizi ya kijeshi siku ya Ijumaa. (12.12.2014) Mabilioni kadhaa ya fedha hizo zimetengwa makhususi kupambana na kundi la Dola la Kiislamu, IS.  Bunge la Marekani liliidhinisha muswada wa sheria kuhusu matumizi makubwa ya ulinzi siku ya Ijumaa yanojumuisha kuimarisha mashambulizi ya kutokea angani dhidi ya kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu, pamoja na kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Iraq na waasi wa Syria. Sheria hiyo, iliyopitishwa kwa kura 89 dhidi ya 11 katika baraza la seneti, inajumuisha ombi la rais wa Marekani Barack Obama la dola bilioni 5 kukabiliana na Dola la Kiislamu. Dola bilioni 3.4 kati ya kiwango hicho zitatengwa kwa ajili ya kuwapeleka wanajeshi wa Marekani kama sehemu ya harakati maalumu iliyopewa jina Operation Inherent Resolve, na dola bilioni 1.6 zitatumika kuwapa vifaa na kuvipa mafunzo vikosi vya Kikurdi kwa miaka miwili. "Mashambulizi ya angani ya Marekani yali

Arsenal,Mancity na Chelsea kuendeleza kipute leo

Picha
Mshambiliaji wa Chelsea Diego Costa Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey hatacheza katika mechi dhidi ya Newcastle hii leo swala lililomlazimu kocha Arsena Wenger kumuita Francis Coquelin ambaye anaichezea kilabu ya Charlton kwa mkopo ili kuchukua mahala pake. Walinzi Laurent Koscielny na nacho Monreal wana majeraha huku Calum Chambers akikabiliwa na marufuku ya mechi moja. Mshambuliaji wa Arsena Alexi Sanchez    Cesc Fabregas ana marufuku ya mda lakini Nemanja Matic yuko tayari kuchukua mahala pake baada ya kuhudumia marufuku ya mda na hivyobasi kukosa mechi dhidi ya Newcastle ambapo Chelsea ilipoteza kwa mara ya kwanza tangu ligi hiyo ianze. Kipa wa Chelsea apata jaraha Kwa upande mwengine mlinda lango wa timu ya Leicester Ben Hamer ataanza kwa mara ya pili katika msimu huu wa EPL katika mahala pa Kasper Schmeichel ambaye anauguza jereha. Nahodha wa kilabu ya Manchester City Vincent Kompany anatarajiwa kucheza kat

Bensouda kusitisha uchunguzi Darfur

Picha
Mwendesha mashtaka mkuu kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita Fatou Bensouda amesema kuwa atasitisha uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita ulioendeshwa katika eneo la Darfur nchini Sudan kutokana na ukosefu wa usaidizi kutoka kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa. Kwenye taarifa yake kwa baraza hilo mwendesha mashtaka huyo amesema kuwa wanawake na wasichana wanaendelea kuathirika zaidi katika jimbo hilo. Rais wa Sudan Omar El Bashir anayetafutwa na mahakama ya ICC kwa kuhusishwa na uhalifu dhidi ya binaadamu katika eneo la Darfur Amesema kuwa kutokuwepo kwa hatua zozote kutoka kwa baraza la umoja wa mataifa kumechangia kuendelea kwa uhalifu na sasa amelazimika kutumia raslimali za mahakama hiyo kwa masuala mengine. Mwaka 2009 mahakama ya ICC ilimhusisha rais wa Sudan Omar al-Bashir na uhalifu wa kivita kwenye jimbo la Darfur lakini hadi sasa hajakamatwa wala hata mmoja wa washirika wake.

Mgogoro kufunga Bunge la EALA

Picha
Spika wa Bunge wa EALA Margeret Zziwa  Bunge la jumuiya ya Afrika mashariki huenda likafungwa iwapo baadhi ya viongozi wakuu wa Afrika mashariki hawataingilia kati kufuatia migogoro ya takriban miezi sita sasa inayolikumba. Hali hiyo inatokana na kwamba mataifa yaliowachagua viongozi hao kama wawakilishi wake hayana uwezo wa kuwaadhibu wabunge hao kulingana na Gazeti la jumamosi la The Citizen nchini Tanzania. Bunge la Tanzania limekiri kwamba halina uwezo wa kuwasimamisha kazi wawakilishi wake katika bunge hilo ,licha ya kwamba wanaendelea kuzozana. Hatua hiyo inajiri baada ya chama cha FDC nchini Uganda kulitaka bunge la nchi hiyo kuwafuta kazi wawakilishi wake kwa kuwa wabunge hao hawatekelezi wajibu wao.     Bendera za maitaifa wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki  Bunge la EALA limeshindwa kufanya kazi katika miezi iliopita huku wanachama wakiwa na mpango wa kumuondoa Spika wa bunge hilo Maregeret Zziwa kwa madai kwamba ameshindwa kutekeleza wajibu wake ina

Rushwa kuinyima misaada Tanzania

Picha
Mbunge Zito Kabwe mwenyekiti wa kamati iliyowasilisha ripoti kuhusu sakata ya Escrow Serikali ya Tanzania iko hatarini kukosa dola za Marekani milioni mia saba sawa na trilioni 1.1 kwa fedha za Tanzania kwa ajili ya mradi wa pili wa mfuko wa changamoto za Milenia (MCC) kutokana na kushamiri kwa vitendo vya rushwa nchini humo. Marekani imebainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo. Haya yanajiri wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo yaliyofikiwa na Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kaunti ya Tegeta Escrow wiki ijayo. Katika tamko hilo kwa umma ambalo limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza kutambua umuhimu wa kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya Tanzania Desemba 9, mwaka huu kwamba itachu

Mshindi wa pili wa bajaji kwenye shinda na serengeti apatikana

Picha
Meneja wa Bia chapa ya Serengeti, Rugambo Rodney katikati akithibitisha namba ya simu ya mkononi ya mshindi wa Limo Bajaj, wakati wa kuchezesha droo hiyo ya “tutoke na Serengeti” (kulia) ni Mkaguzi toka michezo ya kubahatisha , Abdallah Hemedy, na kushoto ni Mkaguzi toka Pricewatercoopers, Golder Kamuzora. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya Serengeti jijini Dar es Salaam. Mkaguzi toka Pricewatercoopers, Golder Kamuzora akithibitisha namba ya mshindi wa Limo bajaji, wakati wa kuchezesha droo ya kumtafuta mshindi wa pili wa limo bajaj, katikati ni Meneja wa Bia chapa ya Serengeti, Rugambo Rodney na kulia ni Mkaguzi toka bodi michezo ya kubahatisha , Abdallah Hemedy, hafla hiyo ilifanyika Serengeti mjini Dar es Salaam. Meneja wa bia chapa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney ,akiongea kwa simu na mshindi wa Limo bajaj ya Pili kutolewa katika shindano la “Tutoke na Serengeti” Peter Emanuel mkazi wa Rombo Kilimanjaro katika shindano linaloendeshwa na ka mpuni hiyo ya bia ya Serengeti. K