Polisi wapokea msaada wa kompyuta
ASKOFU wa Kanisa la Anglikana
Dayosisi ya Tarime, Dk. Mwita Akiri, ametoa msaada wa kompyuta pamoja na
mashine ya kudurufu kwa Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Polisi la jinsia
kwa ajili ya kusaidia utunzaji wa takwimu na ukatili na kuratibu masuala
mbalimbali.ASKOFU wa Kanisa la Anglikana
Dayosisi ya Tarime, Dk. Mwita Akiri
Akikabidhi msaada huo wenye thamani
ya Sh milioni 1.2, Askofu Akiri alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa ajili ya
kuimarisha jitihada za jeshi hilo katika kukomesha vitendo vya ukeketaji watoto
wa kike unaoendelea wilayani Tarime.
Alisema kama viongozi wa kanisa
wanaamini kuwa mila ya kukeketa huathiri afya na maumbile ya watoto wa kike
ambao ni watoto wa Mungu na inapaswa kukomeshwa hivyo kuwashauri wazee wa mila
kusaidia kuzuia mila hiyo.
Makabidhiano hayo yamefanyika jana Kituo
cha Polisi wilayani Tarime na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wilaya ya
Tarime, Issa Bukuku mbele ya Kaimu Mkuu wa Wilaya, Jonathan Machango pamoja na
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi wa Tarime na Rorya, Lazaro Mambosasa.
Kwa upande wake Kamanda wa Kanda Maalumu,
Mambosasa alishukuru kupatikana kwa masada huo na kuongeza kuwa vifaa hivyo
vitasaidia Jeshi la Polisi kwa ujumla kuboresha huduma zake ikiwa ni pamoja na
utunzaji wa kumbukumbu.
Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya, Jonathan
Machango, ambaye pia ni Ofisa Tarafa Mkuu alisema kuwa vifaa hivyo vitumike
vyema na kutekeleza majukumu kama ilivyo kusudiwa.-mtanzania
Maoni
Chapisha Maoni