Mbaroni kwa kukutwa na meno ya tembo
JESHI la Mkoa wa Katavi linawashikilia watu wawili
kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo vipande 22 vya uzito wa kilogramu 46
yenye thamani ya Sh milioni 157.5.
Imeelezwa kutokana na uzito huo, imebainika ni sawa
na tembo saba waliouawa wakati wakiwa
wanataka kuyasafirisha kwenye basi
kutoka Mpanda kuelekea mkoani Kigoma.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi,
Rashid Mohamed, aliwataja watuhumiwa hao
waliokamatwa kuwa ni Justine Baluti (Zolros) (39) mkazi wa Kijiji
cha Ivungwe makazi ya wakimbizi ya
Katumba Wilaya ya Mlele na Bobifaphace Hoza
(40) mkazi wa Kalele Wilaya ya Kasulu
Mkoa wa Kigoma.
Alisema watuhumiwa hao wote wawili walikamatwa jana
saa 12 wakiwa katika harakati za kusafirisha meno hayo katika Stendi ya mabasi
ya Mpanda.
“Siku hiyo ya tukio majira hayo ya saa kumi 12
asubuhi, askari polisi walikuwa doria kwenye eneo la stendi ya mabasi ya Mpanda
yaendayo mikoani, walimtilia shaka mtuhumiwa Justine Baluti aliyekuwa anapakia mizigo yake kwenye basi la
Kampuni ya Adventure lenye namba za usajili
T.992 BUT lililokuwa likielekea mkoani Kigoma.
“Baada ya polisi kumtilia mashaka mtuhumiwa huyo na
yeye alipowaona polisi kwenye eneo hilo alitaka kutoroka, hata hivyo
walifanikiwa kumweka chini ya ulinzi.
“Ulianza upekuzi katika mizigo yake na kumkuta akiwa
na meno ya tembo vipande 15 yenye uzito
wa kilogramu 33 vyenye thamani ya shilingi
milioni 90,” alisema Kaimu Kamanda
Mohamed.-mtanzania
Maoni
Chapisha Maoni