Jaribio la kuiba sanamu la Bikira Maria lakwama
VIJANA wa tatu wakazi wa Mtaa wa Luwawasi, Manispaa ya Songea, wametakiwa kwenda na wazazi wao kutubu
dhambi za kutaka kuiba mapambo ya kanisa pamoja na sanamu ya Bikira Maria
katika Kanisa Katoliki la Kigango cha Samora.
Akizungumzia tukio hilo katika ibada ya Sikuku ya Krismasi iliyoongozwa na Padri Cristom Kapinga na Katekista wa kigango hicho, Keneth Mhagama walisema vijana hao walifanya jaribio hilo usiku wa manane baada ya ibada ya mkesha kumalizika.
Mapambo hayo pamoja na sanamu inayomuonesha mtoto Yesu
vilipambwa kwa ajili ya sherehe za Krismasi.
Akizungumzia tukio hilo katika ibada ya Sikuku ya Krismasi iliyoongozwa na Padri Cristom Kapinga na Katekista wa kigango hicho, Keneth Mhagama walisema vijana hao walifanya jaribio hilo usiku wa manane baada ya ibada ya mkesha kumalizika.
Mhagama alisema kuwa kilichosaidia washindwe kufanya
uharifu ndani ya kanisa hilo ni kutokana na kigango hicho kuweka walinzi ambao
walifanikiwa kuwadhibiti wahalifu hao ambapo baada ya kuwatia mbaroni katika
maelezo yao walijitambulisha majina yao na eneo wanaloishi kuwa ni Mtaa wa Luwawasi.
“Tunawataka hao vijana waje kutubu dhambi zao pamoja na na wazazi wao ili tuweze kumaliza suala hili kiroho na hata kuwanja katika misingi ya kumjua Mungu.
“Tunawataka hao vijana waje kutubu dhambi zao pamoja na na wazazi wao ili tuweze kumaliza suala hili kiroho na hata kuwanja katika misingi ya kumjua Mungu.
“Inaweza kuwasaidia na hata kuachana na tabia hii ya wizi
na kama hawatatii hili basi tutaacha mkono wa sheria uweze kufanya kazi yake,”
alisema Padri Kapinga.
Watuhumiwa hao walitajwa ndani ya Kanisa kwa jina moja moja
kuwa ni Mohamed, Ahmad na Leornad ambao wote ni wakazi wa Luwawasi ambao pamoja
na kudhibitiwa na vijana wa ulinzi walifanikiwa kung’oa koki ya bomba la maji katika
kikango hicho.-mtanzania
Maoni
Chapisha Maoni