Rais wa Nigeria ampendekeza makamu wake kuwa mgombea mwenza
Rais Jonathan amemtaja mgombea mwenza baada ya kukubali uteuzi kuwa
mgombea pekee wa urais kutoka chama tawala nchini Nigeria, PDP, katika
mkutano maalum wa chama uliofanyika jana jioni mjini Abuja.
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ametangaza kuwa, anampendekeza makamu wake Namadi Sambo kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Februari mwaka ujao.
Awali, kulikuwa na tetesi kuwa rais Jonathan angeteua mgombea mwenza mwingine. Sambo alishika madaraka ya makamu wa rais mwaka 2010, na baadaye kuchaguliwa na rais Jonathan kuwa mgombea mwenza kwenye uchaguzi wa mwaka 2011.
Maoni
Chapisha Maoni