Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2014

Zanzibar Heroes wasitisha mazoezi

Picha
TIMU ya Taia ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes'imelazimika kusitisha mazoezi kwa muda kutokana na kile kilichodaiwa kuwa hakuna uhakika juu ya kufanyika kwa mashindano ya challenji. Kocha mkuu wa timu hiyo Hemed Suleiman Moroko ambaye alisema kuwa wameamua kusitisha mazoezi ya timu hiyo kwa muda mpaka pale watakapo pata jibu muafaka kuhusu kufanyika kwa mashindano hayo. Kikosi cha Zanzibar Heroes Alisema kuwa kwasasa itakuwa ni vigumu kuwafanyishamazoezi wachezaji huku kukiwa hakuna uhakika wa mashuindanoyenyewe kwani kufanya hivyo kutawachosha hata wachezaji wenyewe,huku akiongeza kuwa mashindano hayo kwani pia yasipofanyika itakuwa ni hasara kubwa kwa zanzibar kutokana na timu hiyo kushiriki mashindano hayo pekee kwa mwaka mzima.

Amnyonga mkewe,naye ajinyonga

Picha
MUME amemuua mkewe kwa kumnyonga shingo na kisha nayeye kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani, Mwamke huyo Tano Matuma(36)na mumewe Nyikabura Kina(49)wote wakazi wa Sirorimba,kata ya Buswahili,Tarafa ya kiagata wilayani Butiama . Inaelezwa kuwa Tano hakuacha ujumbe wowote unaoeleza sababu za kutenda mauaji hayo na hakuna mtu aliyeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo. Katika tukio jingine mtu mmoja asiyefahamika anaekadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 17-20 amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa mawe na kukatwa mapanga na watu wasiofahamika baada ya kukutwa akivunja nyumba ili aibe mali.-Uhuru Mkoa wa mara umekuwa ukiripotiwa kwa kuwa na matukio ya kikatili hasa ya watu kujichukulia sheria mkononi.

Michepuko yasababisha ukatili

Picha
KUKITHIRI kwa matukio ya unyanyasaji kwa akina mama kunasababisha baadhi ya wanaume kuwa na wapenzi wengine nje ya ndoa. Kauli hiyo ilitolewa  na Ofisa Jinsia na Uhamasishaji kwa Jamii kutoka Shirika la Agape Aids Control Programme, Mustapha   Isabuda. Alisema katika utafiti wao, wamebaini kuwa sababu kubwa ya wanaume wengi kutelekeza familia zao ni kutokana na kuendekeza michepuko, kitendo ambacho wanawake wanabaki kuwa na mzigo mkubwa wa kulea watoto. “Wanaume acheni michepuko, hii ndiyo sababu kubwa ya familia nyingi kuvunjika, takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia Januari hadi Oktoba, mwaka huu, jumla ya akina mama 274 kutoka halmashauri ya Kishapu na Shinyanga wamefanyiwa ukatili wa kijinsia. “Kutokana na ukatili wa kijinsia, jumla ya watoto 637 wamekosa haki zao za msingi kama elimu, chakula, malazi, matibabu na ustawi wao kwa ujumla kutokana na kina baba kuwatelekeza wake zao,” alisema Isabuda. Naye Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Shirika hilo,

Emerson atumia dk 15 kutoa darasa Jangwani

Picha
KIUNGO mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Rogue, ametumia dakika 15 tu kuwatoa nishai baadhi ya wachezaji wavivu wa timu hiyo ambao hawakuweza kwendana na kasi yake. Emerson aliyewasili nchini Jumatano tayari kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga, alianza mazoezi na wenzake juzi na kuendelea jana kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, Dar es Salaam. Baada ya kuanza kwa kuzunguka uwanja mara kadhaa, Mbrazil huyo alipata fursa ya kuingia uwanjani kujumuika na wenzake, ambapo alicheza kwa takribani dakika 15 na kuonyesha mambo ambayo ni wazi yataendelea kuwatesa mno wenzake, hasa wale wavivu wa mazoezi na wasiopenda kufuata maagizo ya makocha wao. KIUNGO mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Rogue, ametumia dakika 15 tu kuwatoa nishai baadhi ya wachezaji wavivu wa timu hiyo ambao hawakuweza kwendana na kasi yake. Unajua ilikuwaje? Kila Emerson alipopata mpira, hakutaka kuremba zaidi ya kutoa pasi na kuomba, akifanya hivyo kwa kasi. Lakini wengi wa wachezaji aliokuwa akiw

Maximo amtaka Traore wa El Merreikh

Picha
KOCHA wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo, ameutaka uongozi wa klabu hiyo kufanya kila linalowezekana kumsajili mshambuliaji raia wa Mali, Mohamed Traore, anayekipiga katika klabu ya El Merreikh ya Sudan. Traore ametokea kuzivutia klabu kadhaa ambazo zinaiwania saini yake, ikiwamo Azam ya Tanzania inayodaiwa kuanza mazungumzo naye. Mohamed Traore Habari kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, zinasema kuwa Maximo anamtaka mshambuliaji huyo ili kuziba nafasi ya Mbrazil mwenzake, Geilson Santos ‘Jaja’ aliyejiengua kutokana na kile alichodai kukabiliwa na matatizo ya kifamilia. Japo Maximo ametua nchini na Emerson Oliveira Neves Rogue, bado atakuwa akihitaji mshambuliaji mahiri wa kati kwani Mbrazil huyo ni kiungo. Pamoja na kiu yake ya kumnasa Traore, bado Maximo hana uhakika wa hilo kwani mshambuliaji huyo analipwa fedha nyingi mno na El Merreikh hivyo Yanga watatakiwa ‘kuvunja benki’ kumng’oa katika klabu hiyo ya Sudan. “Kocha amesema anamtaka Traore, sijui itakuwaje kwani k

Phiri: Sserunkuma ni mashine

Picha
Kocha wa Simba Mzambia Patrick Phiri amesema mshambuliaji mpya wa Simba, Mganda Daniel Sserunkuma, ni mashine na kwamba ataisaidia mno timu hiyo kuipachikia mabao katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Daniel Sserunkuma, Sserunkuma tayari amemalizana na Simba baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo na kusaini mkataba wa miaka miwili. Phiri alisema amemfuatilia Sserunkuma katika mechi alizocheza akiwa na timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ na kubaini ni mshambuliaji wa maana ambaye atawasaidia. Phiri alisema ameangalia video na mechi mbalimbali alizocheza Sserunkuma akiwa na The Cranes pamoja na zile za Ligi Kuu Kenya akiwa na klabu ya Gor Mahia na kubaini Mganda huyo ni moto wa kuotea mbali. Alisema anaamini iwapo watafanikiwa kummiliki mshambuliaji huyo, Simba haitakamatika katika mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara. “Daniel ni mchezaji mzuri, nimemfuatilia akiwa katika timu yake ya Taifa na hata akiwa Gor Mahia kule Kenya,

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4

Picha
Ilipoishia Mwalimu Magdalena alikimbia huku akipiga kelele bila kujua anakokimbilia angepata msaada ama la! Alishaanza kuchoka na ilikuwa giza sana, lakini alichoambulia kugundua ni kwamba mtu aliyekuwa akimkimbiza alikuwa amevaa kinyago na nguo nyeusi ili asitambulike. Sasa Endelea GHAFLA mwalimu Magdalena akajikuta akikamatwa na kufumbwa mdomo, alikukuruka ili ajitoe katika mikono iliyombana vema, lakini hakuweza kuitoa, alijitahidi kujitoa mbele ya mtu huyo aliyemfumba mdomo, sauti pia miguu yake havikumsaidia kufanya chochote kujikwamua kutoka eneo hilo. Mwenyekiti alishangaa kutosikia sauti ya mwalimu Magdalena, akaangaza huku na kule, lakini hakuweza kutambua wapi alipo mwalimu Magdalena, alinyanyua macho huku na huko, lakini hakufanikiwa. Taratibu Mwalimu Magdalena alikuwa akipoteza nguvu kutokana na kubanwa na asiyemjua, mtu yule alimvuta eneo lingine ili kumkwepa mwenyekiti aliyekuwa akimsaka mwalimu Magdalena ili atimize ahadi yake. Mwenyekiti alianza kuhama

Mataifa kumi ya Afrika kwenye viwango vipya vya FIFA

Picha
Taifa hilo limepanda nafasi 17 katika orodha hiyo ya dunia hadi nafasi ya 38 huku wakipanda hadi katika nafasi ya 6 kutoka ya 11 barani afrika. Guinea ndio taifa la Afrika ambalo limepanda juu zaidi katika orodha ya FIFA duniani mwezi wa Novemba. Kuimarika kwa Guinea kunatokana na ushindi wao dhidi ya Togo na Uganda ambo uliwasaidia kufusu katika kombe la Afrika mwaka 2015. Mali ambayo pia ilifuzu katika michuano hiyo ya Afrika ilipanda nafasi tisa zaidi hadi nafasi ya 49 duniani na kuorodheshwa ya 10 barani Afrika. Hatahivyo Misri ilipoteza nafasi 22 na hivyobasi kushuka hadi nafasi ya 60 duniani na 14 barani Afrika. Kwa jumla matokeo hayo yalikuwa mazuri kwa soka ya Afrika,huku mataifa 10 kutoka bara hili yakiorodheshwa katika nafasi hamsini bora duniani. Mataifa 10 bora ya Afrika katika orodha ya FIFA duniani. 1. Algeria (18) 2. Tunisia (22) 3. Ivory Coast (24) 4. Senegal (35) 5. Ghana (37) 6. Guinea (38) 7. Cape Verde (39) 8. Cameroon (41) 8. Senegal (41)

CHIPUKIZI:Wasanii wanashindwa kuwatumia mameneja

Picha
‘Belays ' Abel Gabriel : SANAA ya muziki wa Tanzania inazidi kukua na kutanuka kila siku na ndio maana kukicha inazidi kujinyakulia umaarufu nchini huku idadi ya wafuasi wake ikizidi kuoongezeka licha ya kukumbana na changamoto.   Leo tunaye msanii chipukizi wa miondoko ya Rap Abel Gabriel ‘Belays’ mwenye ndoto za kuja kuwa staa mkubwa kwenye muziki huu. Tangu akiwa shule ya msingi huko mkoani Kigoma hadi sasa ana nyimbo tatu mkononi ambazo ni ‘Niwe nawe, Hujachelewa aliyoirekodi kwenye studio za Say Rekodi na ile ya ‘Waweza kwenda aliyoirekodi kwenye studio za Pamoja Records ambazo alianza kurekodi rasmi mwaka huu.   Belays anasema kuwa licha ya mameneja kuwa tatizo kubwa kwao kutokana na kushindwa kuwapata lakini anadai kuwa wasanii wengi wanapowapata wasimamizi hao (meneja), wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kutokana na kutokuelewa namna ya kuwatumia meneja huo kwani wengi hushia kunyonywa tu na hao mameneja.   “Wasanii wengi tunashindwa kufikia kilele cha mafani

Wakenya waandamana kudai usalama uimarishwe

Picha
Wakenya waliandama mjini Nairobi siku ya Jumanne hadi ofisi ya rais kudaia kufukuzwa kwa waziri wa mambo ya ndani na mkuu wa polisi kutokana na kuzorota kwa usalama nchini humo, hasa baada ya kuuliwa kwa watu 28 huko Mandera na wapiganaji wa Kisomali - al-Shabab.  Muandamanaji amelalia misalaba iliyopakwa rangi nyekundu kudai usalama zaidi Waandamanaji wakiimba kutaka usalama zaidi Kenya Waandamanaji wakimbia wakiacha majeneza baada ya kufurushwa na Polisi Nairobi Waandamanaji waweka misalaba mwekundu kuonesha idadi ya walofariki kutokana na ghasia Kenya Waandamanaji wakiimba kudai kuimarishwa kwa usalama na kuondolewa wakuu wa usalama Waandamanaji wabeba majeneza ikimaanisha wamechoka kuwazika watu walouliwa wasio na hatia Polisi wa Kenya wafyetua mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji Nairobi

Waliopeperusha bendera ya ’Yaa Hussein’ wafungwa Saudia

Picha
Vijana watano nchini Saudi Arabia wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 21 na miezi 6 jela kila mmoja kwa kosa eti la kupeperusha bendera iliyoandikwa ‘Yaa Hussein’ nchini humo. Ahmad ar Rabbah mwanaharakati na mkuu wa Taasisi ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Saudi Arabia amelaani vikali adhabu hiyo dhidi ya vijana hao Waislamu wa Madhehebu ya Shia na kusisitiza kuwa, kitendo hicho kinakiuka misingi ya haki za binadamu. Rabbah amesisitiza kuwa, adhabu hiyo haina mfungamano wowote na sheria za ndani ya nchi hiyo wala za kimataifa, bali inaonyesha chuki za wazi na ubaguzi wa kimadhehebu unaofanywa na utawala wa kifalme wa Aal Saud dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. utawala wa Saudi Arabia mara kwa mara umekuwa ukitoa adhabu ya vifo au vifungo vya muda mrefu dhidi ya maulamaa, waandamanaji na wafuasi wa madhehebu ya Ahlul Bayt AS nchini humo. Imam Hussein bin Ali bin Abi Talib AS, ni mjukuu wa Mtume Mtukufu Muhammad SAW.

Bahrain kuwachukulia hatua waliosusia uchaguzi

Picha
Waziri wa Sheria wa Bahrain ametaka watu wote waliokataa kushiriki kwenye uchaguzi wa Bunge uliofanyika hivi karibuni nchini humo kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Khalid bin Ali Aal Khalif Khalid bin Ali Aal Khalifa ameyasema hayo mbele ya kikao cha baraza la mawaziri kilichofanyika mjini Manama. Pendekezo hilo la Waziri wa Sheria wa Bahrain la kuchukuliwa hatua wale wote waliokataa na kususia uchaguzi wa Bunge, tayari limewasilishwa mbele ya kamati ya sheria ya baraza la mawaziri. Imeelezwa kuwa, duru ya kwanza ya uchaguzi wa Bunge wa kimaonyesho iliyofanyika siku ya Jumamosi iliyopita nchini Bahrain, iliwashirikisha watu laki tatu na elfu hamsini. Duru ya pili ya uchaguzi huo, imepangwa kufanyika Jumamosi ijayo. Serikali ya Bahrain ilitangaza kwamba asilimia 51.5. ya watu waliotimiza masharti ya kupiga kura walishiriki kwenye uchaguzi huo, ilhali, chama kikuu cha upinzani cha al Wifaq nchini Bahrain kilitangaza kuwa, karibu asilimia 30 tu ya watu ndiyo iliyoshi

Makamu wa Rais Zimbabwe atimuliwa ndani ya chama

Picha
Makamu wa Rais wa Zimbabwe Joice Mujuru ambaye anatuhumiwa kupanga njama ya kumpindua Rais Robert Mugabe leo amevuliwa ustahiki wa kuwania uanachama katika kamati kuu ya chama tawala ZANU-PF. Nyaraka alizowasilisha Mujuru kwa ajili ya kuwania uanachama katika kamati hiyo muhimu zimekatiliwa na kamati ya utendaji. Hatua hiyo inakuja kabla ya kongamano la kitaifa la ZANU-PF ambalo limepangwa kufanyika wiki ijayo. Katika siku za hivi karibuni magazeti yaliyo karibu na Rais Mugabe yamekuwa yakimtuhumu Mujuru kuwa anapanga njama za kumuondoa Mugabe madarakani. Hivi sasa kuna mvutano mkubwa katika chama tawala kuhusu ni nani atakayechukua nafasi ya Mugabe mwenye umri wa miaka 90 endapo atajiuzulu au afariki dunia. Novemba 17 Mujuru alijitetea na kusema hajahusika na njama zozote za kutaka kumuua Rais Mugabe. Imedokezwa kuwa Mujuru na Waziri wa Sheria Emmerson Mnangagwa, ndio wanasiasa waandamizi wanaowania kuchukua nafasi ya Mugabe ambaye ameitawala Zimbabwe tokea mwa

Wasichana Kenya watumia miili yao kujikimu kimaisha

Picha
Wasichana wadogo nchini Kenya wamekuwa wakilazimika kujiingiza katika unywaji pombe na uuzaji wa miili yao kama njia ya kujipatia chakula wao na familia zao. Brittanie Richardson binti wa kimarekani mwenye umri wa miaka 27 ameanzisha kampeni ya kupinga hali hiyo baada ya ziara yake iliyoshuhudia vitendo hivyo vya mara kwa mara kwa familia zilizo na hali ngumu ya maisha. Mjini Nairobi kuna msongamano mkubwa wa makazi duni, watoto wenye njaa mara nyingi wanafanya biashara ya miili yao ili kujipatia pesa kidogo au chakula, mji huo wenye wakazi milioni 3.1, ni nyumbani kwa watu milioni 2 wanaoishi katika makazi duni na idadi ya watu katika makazi duni katika mji huo mkuu wa Kenya inakua kwa asilimia 6 kwa mwaka. Kulingana na shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa Mataifa Kenya ina watoto wanaofanya kazi ya ngono 30,000 waliogawanyika katika pembe zote za fukwe za utalii, huku ukahaba miongoni mwa watoto likitambuliwa kama tatizo linalohitaji kukabiliwa kwa utekelezaji

Daktari wa Congo kukabidhiwa tuzo ya Sakharov

Picha
Tuzo ya Sakharov inayotolewa na Bunge la Ulaya kwaajili ya utetezi wa haki za binaadamu inakabidhiwa kwa daktari wa nchini Congo Dr Denis Mukwege kwa kazi yake ya kuwasaidia maelfu ya waathiriwa wa ubakaji nchini humo. Daktari Dennis Mukwege Daktari Mukwege amekabidhiwa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kuwasaidia wanawake wanaopitia visa vya unyanyasaji wa kingono katika maeneo ya kivita. Mwaka wa 1998 Mukwege aliye na umri wa miaka 59 alianzisha hospitali yake ya Panzi mjini Bukavu nchini Congo na hadi sasa bado anaendeleza juhudi zake za kuwasaidia waathirika wa ubakaji. Na ndio maana tarehe 21 mwezi Oktoba mwaka huu, bunge la Ulaya likaamua kumtambua Daktari huyo kwa kumtangaza mshindi wa tuzo hiyo ya Sakharov anayokabidhiwa rasmi hii leo mjini Strasbourg, Ufaransa. "Tunatarajia kupata suluhu ya kusimamisha ubakaji kutumiwa kama ngao katika vita na wakati mwengine kama mkakati wa kuanzisha vita." Alisema daktari Dennis Mukwege ambaye licha ya ku

Aomba ndevu zipigwe marufuku katika soka

Picha
Wanamichezo wanaongoza katika orodha ya watu ambao huwa kati mstari wa mbele katika fesheni, iwe ni nguo ama hata utengezaji wa nywele. Ni mabingwa katika kuwa na nywele zilizotengezwa vizuri ama hata ufugaji wa ndevu. Lakini afisa moja wa soka nchini Uturuki yuko katika harakati ya kupiga marufuku mpango huo. Ilhan Vacvac,mwenyekiti wa kilabu ya Uturuki ya Genclerbirligi ametangza vita dhidi ya wanasoka wanaovuga ndevu. ,la kushangaza ni kwamba yeye mwenye anafuga masharubu. Amesema kwamba mchezaji yeyote atakekuka marufuku hiyo ikiwemo wachezaji na mameneja watapigwa faini ya shilingi milioni 1.02 fedha za kenya . Amesema kuwa yeye mwenyewe licha ya kuwa na umri wa miaka 80 hunyoa ndevu zake. Anasema kwa kuwa mchezaji ni sharti mtu awe mfano mwema kwa vijana.Cavcav alinukuliwa akiliambia gazeti la Uingereza la the Gurdian. Akiongezea kuwa ndevu hizo huwafanya wachezaji hao wa soka kuwa kama wanafunzi. Inadiwa kuwa bwana Cavcav amejaribu kulishawishi shirikisho la so

Ajali ya Hiace yaua 9

Picha
WATU tisa wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa vibaya, baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 761 CKD kupinduka. Basi hilo liligonga tuta la barabarani na kupoteza mwelekeo kisha kutumbukia mtaroni katika eneo la Buhangija mkoani Shinyanga. Tukio hilo limetokea leo saa 4 asubuhi wakati Hiace hiyo ikitoka Kahama kwenda Shinyanga. Mashuhuda wa ajali hiyo, walisema dereva wa gari hilo, Anuari Awadhi (42) alikuwa anaendesha kwa mwendo kasi, ghafla akakutana na tuta ambalo lilisababisha kupoteza mwelekeo na kupinduka mara tatu ambapo abiria watano walifariki dunia papo hapo. Shuhuda wa ajali hiyo, Budoya Machiya, amesema gari hilo lilikuwa likifukuzana na Toyota Hiace nyingine na kwamba baada ya ajali dereva alikimbia kusikojulikana. “Ajali imetokea kutokana na mwendo kasi wa gari, dereva alikuwa anafukuzana na Hiace nyingine, akagonga tuta na gari letu lililokuwa nyuma likatumbukia mtaroni,”  Emmanuel John. Mganga Mfawidhi wa Hospital

Jengo laua Kumi Misri

Picha
Watu kumi wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa kuanguka mjini Cairo nchini Misri, maafisa wameeleza. Watu saba wamejeruhiwa baada ya jengo la ghorofa nane kuanguka usiku. Mkuu wa Idara ya dharula Jenerali Mamdouh Abdul Qader amesema vikosi vya uaokoaji vinawasaka Watu 15 wanaokisiwa kunasa kwenye kifusi. Mara kadhaa majengo yameanguka nchini humo, sababu kubwa ikiwa ujenzi usiofuata kanuni na Sheria pia usimamizi mbovu wa taratibu za ujenzi. Jenerali Qader ameliambia shirika la Habari la Ufaransa kuwa hawajui chanzo cha ajali hiyo,lakini walipatiwa taarifa kuwa ghorofa mbili za juu zilijengwa kinyume cha sheria. Wakazi wa majengo ya karibu na lilipoanguka jengo hilo wameondoka katika makazi yao kwa nia ya kujihadhari. Mwezi Januari Mwaka jana,Watu 28 walipoteza maisha baada ya jengo la ghorofa nane kuanguka mjini Alexandria.

Serikali yatakiwa kudhibiti ulevi Kilimanjaro

Picha
SERIKALI imetakiwa kuingilia kati tatizo la ulevi wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro, kwa kuwa ulevi huo unachangia ongezeko la watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu. Rai hiyoimetolewa leo na Mwenyekiti wa asasi ya jinsia na maendeleo wilayani Rombo (AJIMARO) Athony Massawe, wakati akikabidhi msaada wa chakula kwa watoto yatima na wale wenye maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi katika Kituo  cha Kulelea Watoto kiitwacho Cornel Ngaleku cha wilayani hapa. “Tatizo la ulevi kwa wananchi wilayani hapa, linakua siku hadi siku na ni vema Serikali ikaingilia kati na kulidhibiti, kwani limechangia maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi na kusababisha ongezeko la watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu. “Tatizo hili pia limechangia kiwango cha umasikini kuongezeka kwa wananchi, kwani vijana wengi ambao ndio nguvu kazi ya taifa, wameathiriwa na pombe na wamesahau kufanya kazi kwa ajili ya kujiletea maendeleo. “Kutokana na tatizo hilo, alisema asasi yake imejikita katika ut

Wanawake waandamana kwenda msituni

Picha
ZAIDI ya wanawake 100 wa jamii ya Kimasai wameandamana kwenda kulala msituni kwa siku mbili wakipinga kitendo cha serikali kukata miti ya asili katika Kijiji cha  Matebete, Kata ya Itamboleo, Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya. Wanawake hao walichukua uamuzi huo jana, wakipinga hekta zaidi ya 32,000 za miti wanayoitegemea katika shughuli zao, kukatwa bila wao kushirikishwa.   Mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina la Sofia Kalei, alisema hawako tayari kuona msitu huo ukiteketezwa kwa sababu umekuwa ukiwasaidia katika shughuli mbalimbali.   “Serikali imeamua kukata miti katika msitu huu kwa kisingizio kwamba inataka kutengeneza madawati kwa ajili ya wanafunzi.   “Tukiruhusu miti hii ikatwe, tutakuwa tukijimaliza wenyewe na tutakaoathirika zaidi ni sisi wanawake na siyo watu wengine. “Kwa maana hiyo, ili kuonyesha jinsi tusivyokubaliana na uamuzi huu wa Serikali, tumeamua kuandamana na kuja msituni ili kupinga mpango huo wa Serikali,” alisema Kalei.   Naye M

Wafanyakazi waidai Muhimbili Sh mil 121

Picha
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili inadaiwa zaidi ya Sh milioni 121.5 ambazo ni malimbikizo ya fedha za likizo za wafanyakazi ambao ni wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE). Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Aminieli Eligaesha, amesema uongozi wa hospitali hiyo umeanza kupunguza deni hilo tangu Juni, mwaka huu. “Tumeanza Juni, mwaka huu kupunguza deni hilo ambalo lilitokana na hospitali kutokuwa na fedha za kutosha za kuwalipa, ndiyo maana tumeshindwa kuwalipa kwa wakati,”  Eligaesha. Amesema awali deni hilo lilikuwa kubwa ikilinganishwa na kipindi hiki, lakini uongozi ulifanikiwa kulipunguza. Eligaesha amesema kutokana na hali hiyo, wafanyakazi wote wanaoendelea kuomba likizo hawataweza kulipwa fedha zao hadi deni hilo litakapomalizika. “Kwa wafanyakazi ambao wataomba likizo hawatalipwa fedha zao hadi deni la wafanyakazi wanaodai litakapolipwa,” amesema Eligaesha. Kutokana na hali hiyo, amewasihi wafanyakazi kuwa wavumilivu wakati hu

Shabiki amng'ata mwenziwe Kenya

Picha
Mwanamume mmoja mjini Kisumu Magharibi mwa Kenya, alimng'ata sikio jirani yake baada ya mechi ya soka ya ligi ya uingereza iliyokuwa na matokeo yasiyo ya kuridhisha kwa mmoja wao. Mwanamume huyo ambaye ni shabiki sugu wa klabu ya soka ya Arsenal aliamua kujiondolea hasira ya klabu yake kushindwa na Manchester United kwa kumng'ata hasimu wake wa Man U sikio lake Jumamosi usiku. Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa shabiki huyo sugu wa Arsenal hangeweza kustahimili kukejeliwa na jirani yake shabiki wa Man United baada ya klabu yake kushindwa mabao mawili kwa moja Mwanamume huyo alifungiwa katika chumba kimoja na wakazi wa mtaa wa Railways mjini humo, ambao walitaka kumuua kwa kitendo chake. Inadaiwa hii ni mara ya pili kwa mwanamume huyo kumng'ata mwenziwe sikio kwa sababu za kisoka.

Casillas kuwania tuzo ya kipa bora

Picha
Kipa wa Real Madrid na Uhispania Iker Casillas ameorodheshwa kwa timu ya Fifa World 2014 XI licha maonyesho yake mabaya kwenye Kombe la Dunia na kucheza michezo12 tu ligi.   Iker Casillas Kipa wa Chelsea Thibaut Courtois yuko kwenye orodha hiyo, pamoja na Manuel Neuer wa Bayern Munich,Claudio Bravo wa Barcelona na Gianluigi Buffon wa Juventus. Lakini kujumuishwa kwa Casillas kumeshangaza, licha yake kuwa katika timu kwa miaka mitano tangu 2008-2012. Alicheza mechi mbili tu ya ligi ya La Liga msimu wa 2013-14 na mechi 10 zaidi msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa 33, aliyeinua kombe la Ligi ya Mabingwa na Real, alikosa na kusababisha angalau bao moja katika mechi ya Kombe la Dunia waliocheza Uhispania dhidi ya Uholanzi na Chile, na kuwasababisha kama wamiliki kuondoka baada ya hatua ya makundi. Courtois anaorodheshwa baada ya kuisaidia klabu ya Atletico Madrid ya Hispania kushinda ligi msimu uliopita wakati akiichezea kwa mkopo,aliendelea kuvutia akichezea Belgium

Bunduki bandia yamletea maafa

Picha
Wakili anayewakilisha familia ya kijana mweusi mwenye umri wa miaka kumi na mbili aliyepigwa risasi na polisi katika mji wa Cleveland nchini Marekani, amesema familia yake itafanya uchunguzi wake sambamba na ule unaofanywa na Polisi kubaini kilichotokea. Tamir Rice Kijana huyo kwa jina Tamir Rice mwenye umri wa miaka 12 alikuwa amebeba kile kilichoonekana kuwa bunduki bandia. Polisi wanadai kuwa kijana huyo alikataa kutii amri alipoambaiwa asalimu amri. Kifaa walichokuwa nacho polisi ndicho kilibaini kuwa bunduki hiyo ilikuwa bandia. Inaarifiwa kijana huyo alipigwa risasi mara mbili baada ya kuitoa bunduki yake kiunoni mwake lakini hakujaribu hata wakati mmoja kuielekeza kwa poliso wala kujribu kuifyatua. Wakili wa familia hiyo amesema kuwa ikiwa watapata kuwa haki za kijana huyo zilikiukwa, familia yake itachukua hatua za kisheria dhidi ya polisi. Mwanasiasa mmoja anapendekeza sheria ambayo itahakikisha kuwa bunduki bandia zinakuwa na rangi unayong'aa zaidi ili

Njama ya polisi kumvua mwanamke nguo yatibuka

Picha
Afisa mmoja wa polisi wa utawala nchini Kenya ni miongoni mwa wanaume waliokamatwa kwa kujaribu kumvua nguo mwanamke katika mtaa wa Komarock viungani mwa mji mkuu Nairobi. Polisi walisema watu wanne walimsingira mwanamke huyo alipokuwa anaenda nyumbani kutoka kanisani akiwa ameandamana na rafiki yake. Wanaume hao walijaribu kumvua nguo mmoja wa wanawake hao ila waliokolewa na wananchi waliokuwa wakielekea makwao. Wanaume wawili waliokuwa wanawaokoa wanawake hao walijeruhiwa. Kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa Daily Nation, Kioo cha basi iliyokuwa barabarani pia kilivunjika katika purukushanio hilo. Polisi waliofika katika eneo la tukio waligundua kuwa mmoja wa waliowashambulia wanawake hao alikuwa afisa wa polisi. Tukio hilo limefanyika siku chache tu baada ya mamia ya wanawake kuandamana mjini Nairobi kulaani kitendo cha kumvua mwanamke mmoja mavazi yake yakisemekana kutokuwa na heshima.

Mfanyakazi mkatili matatani

Picha
Polisi nchini Uganda wamebadilisha mashtaka ya mfanyikazi wa nyumbani aliyenaswa kwa kamera akimpiga na kumtendea unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu, kutoka kwa kosa la kutesa na sasa anakabiliwa na kosa la jaribio la mauaji. Video hiyo iliwaudhi watu wengi sana kwenye mitandao ya kijamii ila babake mtoto huyo alisema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha wazazi wenegine. Mfanyakazi huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika gereza la Luzira na mahakama ya Nakawa kwa kosa la kutesa chini ya kifungo cha 41 kwenye katiba kinachoongelea dhidi ya mateso. Mwanamke huyo sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Disemba. Hata hivyo, msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, amesema "shtaka dhidi ya mwanamke huyo lilibadilishwa baada ya kupitiwa mwendesha mkuu wa mashitaka. Tumuhirwe alikubali kosa la kumpiga mtoto huyo kwa kurunzi, tuki olililonaswa kwa kamara ya CCTV. Polisi walimfanyia Tumuhirwe uchunguzi wa kiakili na kubaini kuwa ana akili

Upinzani Nigeria walaani uvamizi

Picha
Chama cha upinzani nchini Nigeria, kimelaani uvamizi uliofanywa na maafisa wa usalama dhidi ya ofisi zake mjini Lagos mwishoni mwa wiki. "Tunataka uchunguzi huru ufanywekubaini sababu zilizopelekea maafisa waliokuwa wamejihami kuvamia ofisi zetu, '' alisema naibu mwenyekiti wa chama cha upinzani cha (APC) Lawal Shuaibu t Chama hicho kilisema ,komputa zake pamoja na nyaraka nyinginezo ziliporwa wakati wa msako huo. Wakuu wa usalama wanasema wanachunguza madai ya chama hicho kutengeza kadi bandia za wapiga kura kabla ya uchaguzi kufanyika mwezi Februari. Maafisa wa usalama walidai kuwa chama hicho kilikuwa kinatengeza kadi bandia kwa lengo la kuvamia mtandao wa tume ya uchaguzi kwa lengo la kubadilisha data ya tume hiyo. Kwa sasa maafisa wa usalama wameweka vifaa vya udukuzi kwa ofisi hio baada ya kuhakikisha kuwa baadhi ya shughuli zinazoendelea katika jengo hilo, zinakwenda kinyume na sheria. Chama hicho kimesema kuwa maafisa wa usalama walitwaa nyara

Chama chamfukuza Rais

Picha
Guys Scott CHAMA tawala cha nchini Zambia cha Patriotic Front (PF) kimemfuta uanachama Rais wa mpito wa nchi hiyo, Guys Scott, kwa madai ya kuvunja taratibu za kikatiba. Kiongozi huyo aliyepewa jukumu la kuiongoza nchi hiyo baada ya kifo cha Rais Michael Sata, anahusishwa na uvunjaji wa taratibu mbalimbali za chama hicho, ikiwa ni pamoja na kufukuza ovyo wafanyakazi. Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa PF, Malozo Sichone, ilieleza Rais Scott amekuwa na tabia ya kuajiri na kufukuza viongozi katika muda mfupi aliokaa katika uongozi wake. “Scott amekuwa na tabia ya kuajiri na kuwafukuza watu kazi ovyo bila ya kushauriana na Kamati Kuu ya chama,” alisema Sichone. Alisema licha ya kutimuliwa ndani ya chama, lakini ataendelea kuwa mwanachama wa chama hicho katika kipindi cha mpito cha urais wake hadi Januari 20, 2015, baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu. Rais Scott hataweza kuwania kiti hicho kupitia PF kutokana na kukosa sifa inayomtaka kuwa na wazazi wazawa wa nchi h

Hadithi:Mwalimu Magdalena sehemu ya 3

Picha
TITLE: Mwalimu Magdalena. SEHEMU ya Tatu.   Ilipoishia kipindi kilichopita... Magdalena, taratibu machozi yalimtoka akamuangalia John naye machozi yalimtoka, akainuka na kumfuata mwalimu Magdalena akaanza kumfuta machozi. Wakati mwalimu Magdalena anasimama ili amshukuru John kwa kumkumbatia, baba yake John anamuona akifanya hivyo, anakasirishwa na jambo hilo anawasogelea. sasa endelea “Huo ndio ualimu wenye weledi, nauliza huo ndiyo weledi, nyie walimu wasichana kwa nini hivi, ni matatizo haujaolewa wewe, umeletwa huku kutufundishia watoto wetu ama kuwaharibu,’’ alifoka mzee Katuba baba wa John. “Mzee kukumbatia si vitu vya kawaida kuna jambo la kusikitisha kanihadithia John nikamkumbatia kwa kumfariji kwani kuna tatizo,’’ alijibu mwalimu Magdalena kwa kusitasita huku akifuta machozi yaliyokuwa yakimtiririka machoni mwake. “Nimesema mambo yenu ya kizungu huko huko mjini kwenu, huku kwetu hatutaki upuuzi wenu kama mmekuja kufundisha mfanye kazi ya kufundisha siyo kuharib

Mama atelekeza watoto wake

Picha
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke linamshikilia mkazi wa Mbagala Kwa Azizi Ally, Mariam Issa, kwa kosa la kutelekeza watoto wake watatu katika kituo cha   Masista Kurasini, kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki mjini   Dar es Salam. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Sabastian Zacharia, alisema mtuhumiwa alikamatwa juzi katika eneo la Kwa Azizi Ally, katika nyumba aliyokuwa akiishi. Alisema taarifa za awali zilizofikishwa kituoni hapo na Masista wa kituo hicho, zilieleza kuwa mama huyo alifika katika kituo hicho   akiwa na wawoto wake kwa lengo la kuomba msaada ili aweze kusaidiwa kulelewa. Alisema mtuhumiwa huyo aliondoka kimyakimya na kuwaacha watoto watatu, akiwamo wa kike mmoja na kutokomea kusikojulikana.   “Watoto hawa ni wadogo, mkubwa ana umri wa miaka mitatu na nusu, wa pili ana miaka miwili na nusu na wa mwisho ana mwaka mmoja na nusu. “Watoto hao baada ya kutelekezwa na mama yao masista wa kituo hicho waliripoti katika kituo chetu cha Polisi hapa C