Ajali ya Hiace yaua 9
WATU
tisa wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa vibaya, baada ya basi dogo la
abiria aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 761 CKD kupinduka.
Basi
hilo liligonga tuta la barabarani na kupoteza mwelekeo kisha kutumbukia mtaroni
katika eneo la Buhangija mkoani Shinyanga.
Tukio
hilo limetokea leo saa 4 asubuhi wakati Hiace hiyo ikitoka Kahama kwenda
Shinyanga.
Mashuhuda
wa ajali hiyo, walisema dereva wa gari hilo, Anuari Awadhi (42) alikuwa anaendesha
kwa mwendo kasi, ghafla akakutana na tuta ambalo lilisababisha kupoteza
mwelekeo na kupinduka mara tatu ambapo abiria watano walifariki dunia papo
hapo.
Shuhuda
wa ajali hiyo, Budoya Machiya, amesema gari hilo lilikuwa likifukuzana na Toyota
Hiace nyingine na kwamba baada ya ajali dereva alikimbia kusikojulikana.
“Ajali
imetokea kutokana na mwendo kasi wa gari, dereva alikuwa anafukuzana na Hiace
nyingine, akagonga tuta na gari letu lililokuwa nyuma likatumbukia mtaroni,”
Emmanuel John.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, Dk. Mfaume Salum, amesema amepokea
maiti tano kutoka eneo la tukio na wengine wanne walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Longinus Tibishubwamu, amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo.
Ambapo amewataja
waliofariki ni Nkingwa Kariagi (50), mkazi wa Mwamanota, Kishapu; Kelvin
Michael (21), utingo wa gari hilo mkazi wa Ngokolo, mjini Shinyanga na Masanilo
Jisandu (miaka 50), mkazi wa Negezi Kalitu, Kishapu.
Wengine
ni Amina Abdallah, mkazi wa Mbika Kahama; Nkola Shija (20), mkazi wa Kahama na Elizabeth
Ngusa (15), mkazi wa Maswa. Wengine watatu hawajajulikana.
Majeruhi katika ajali hiyo ni Peter Yustasi (49),
mkazi wa Sengerema; Frola Ngudungi (35), mkazi wa Ushetu, Kahama; Yesaya Samwel
(40), mkazi wa Singida; Kwimba Damayake (36), mkazi wa Iramba, Tabora; Nyanzobe
Henge (70), mkazi wa Uloa, Kahama; Katumbi Nangi (36), mkazi wa Uloa, Kahama; Emmanuel
John (22) mkazi wa Mwakitolyo; Jimoda Kaliagi (52), mkazi wa Mwamanota, Kishapu
na Kalwa Mwandu (36), mkazi wa Kahama.
Maoni
Chapisha Maoni