Bunduki bandia yamletea maafa

Wakili anayewakilisha familia ya kijana mweusi mwenye umri wa miaka kumi na mbili aliyepigwa risasi na polisi katika mji wa Cleveland nchini Marekani, amesema familia yake itafanya uchunguzi wake sambamba na ule unaofanywa na Polisi kubaini kilichotokea.http://assets.nydailynews.com/polopoly_fs/1.2020966.1416787169!/img/httpImage/image.jpg_gen/derivatives/article_970/tamir-rice.jpgTamir Rice
Kijana huyo kwa jina Tamir Rice mwenye umri wa miaka 12 alikuwa amebeba kile kilichoonekana kuwa bunduki bandia. Polisi wanadai kuwa kijana huyo alikataa kutii amri alipoambaiwa asalimu amri.
Kifaa walichokuwa nacho polisi ndicho kilibaini kuwa bunduki hiyo ilikuwa bandia.
Inaarifiwa kijana huyo alipigwa risasi mara mbili baada ya kuitoa bunduki yake kiunoni mwake lakini hakujaribu hata wakati mmoja kuielekeza kwa poliso wala kujribu kuifyatua.
Wakili wa familia hiyo amesema kuwa ikiwa watapata kuwa haki za kijana huyo zilikiukwa, familia yake itachukua hatua za kisheria dhidi ya polisi.
Mwanasiasa mmoja anapendekeza sheria ambayo itahakikisha kuwa bunduki bandia zinakuwa na rangi unayong'aa zaidi ili ziweze kutambulika haraka.-bbc

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4