Phiri: Sserunkuma ni mashine


Kocha wa Simba Mzambia Patrick Phiri amesema mshambuliaji mpya wa Simba, Mganda Daniel Sserunkuma, ni mashine na kwamba ataisaidia mno timu hiyo kuipachikia mabao katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

http://www.newvision.co.ug/newvision_cms/gall_content/2014/10/2014_10$largeimg206_Oct_2014_183949220.jpg
Daniel Sserunkuma,
Sserunkuma tayari amemalizana na Simba baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Phiri alisema amemfuatilia Sserunkuma katika mechi alizocheza akiwa na timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ na kubaini ni mshambuliaji wa maana ambaye atawasaidia.

Phiri alisema ameangalia video na mechi mbalimbali alizocheza Sserunkuma akiwa na The Cranes pamoja na zile za Ligi Kuu Kenya akiwa na klabu ya Gor Mahia na kubaini Mganda huyo ni moto wa kuotea mbali.



Alisema anaamini iwapo watafanikiwa kummiliki mshambuliaji huyo, Simba haitakamatika katika mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara.

“Daniel ni mchezaji mzuri, nimemfuatilia akiwa katika timu yake ya Taifa na hata akiwa Gor Mahia kule Kenya, huyu ni mshambuliaji aliyekamilika… naamini atatusaidia sana,” alisema.

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Phirifour(1).jpg
Patrick Phiri
Sserunkuma alijiunga na Gor Mahia katikati ya msimu wa 2012, akitokea Nairobi City Stars ambapo katika msimu wake wa kwanza na timu hiyo, alifunga mabao 16 katika Ligi Kuu Kenya na kuiwezesha kutetea ubingwa wao wa ligi hiyo.



Katika hatua nyingine, Mzambia huyo, amesema ameanza maandalizi kabambe kuhakikisha wanashinda mechi ya Nani Mtani Jembe 2 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, itakayochezwa Desemba 13, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Alisema baada ya Yanga kushindwa kuwafunga katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara iliyochezwa Oktoba 18, mwaka huu kwa kutoka suluhu, watawashikisha adabu watani wao hao kwenye mechi hiyo ya Nani Mtani Jembe.

Phiri alisema wameanza kujipanga kwa mazoezi makali ya viungo katika klabu ya mazoezi (gym) ya Chang’ombe, Dar es Salaam kwa ajili ya kuwajengea nguvu ya mwili wachezaji wake.

“Mechi inayokuja dhidi yetu na Yanga hakuna droo tena, Simba ni timu kubwa tunahitaji kushinda,” alisema Phiri.

Katika mikakati hiyo, amepanga kucheza mechi mbili za kirafiki baada ya wachezaji kuingia kambini kuanzia wiki ijayo.-bingwa


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4