Emerson atumia dk 15 kutoa darasa Jangwani

KIUNGO mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Rogue, ametumia dakika 15 tu kuwatoa nishai baadhi ya wachezaji wavivu wa timu hiyo ambao hawakuweza kwendana na kasi yake.
Emerson aliyewasili nchini Jumatano tayari kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga, alianza mazoezi na wenzake juzi na kuendelea jana kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, Dar es Salaam.

Baada ya kuanza kwa kuzunguka uwanja mara kadhaa, Mbrazil huyo alipata fursa ya kuingia uwanjani kujumuika na wenzake, ambapo alicheza kwa takribani dakika 15 na kuonyesha mambo ambayo ni wazi yataendelea kuwatesa mno wenzake, hasa wale wavivu wa mazoezi na wasiopenda kufuata maagizo ya makocha wao.KIUNGO mpya wa Yanga, Emerson Oliveira Neves Rogue, ametumia dakika 15 tu kuwatoa nishai baadhi ya wachezaji wavivu wa timu hiyo ambao hawakuweza kwendana na kasi yake.https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/11/jaja-11.png



Unajua ilikuwaje? Kila Emerson alipopata mpira, hakutaka kuremba zaidi ya kutoa pasi na kuomba, akifanya hivyo kwa kasi. Lakini wengi wa wachezaji aliokuwa akiwapasia, hawakuwa wakimtendea haki kwani mara nyingi waliupokea mpira na aidha kukaa nao kwa muda mrefu au kuurudisha nyuma.

Kitendo hicho kilionekana kumkera Mbrazil huyo kwa kushindwa kurudishiwa pasi aliyotoa, wakati akiwa ameiomba akiwa katika nafasi nzuri.

Kilichoonekana katika mazoezi hayo ya jana, wachezaji wengi wa Yanga hawana elimu ya kutosha juu ya suala zima la pasi fupi fupi na za haraka (one-two).

Ni kutokana na kuonekana kuboreka kwa jinsi baadhi ya wenzake (majina tunayo), Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo aliamua kumpumzisha baada ya dakika hizo 15.

Hadi anatolewa uwanjani, Emerson alikuwa ameshathibitisha kile kinachoonekana katika vipande vya video zake kwenye mtandao vinavyomwonyesha kama kiungo mchezeshaji mwenye uwezo wa hali ya juu.

Kati ya vitu adimu alivyovionyesha jana ni upigaji pasi za haraka, kufungua vyumba, nguvu, wepesi kukaba, kupora mipira na mengineyo kama hayo.

Ni wazi kutokana na mambo yaliyoonyeshwa na Emerson jana, viungo na washambuliaji wa Yanga kama Haruna Niyonzima, Andrey Coutinho, Simon Msuva, Hassan Dilunga, Hamis Thabiti, Mrisho Ngassa, Mbuyu Twite, Jerry Tegete, Said Bahanuzi, Hussein Javu na Nizar Khalfan wanatakiwa kujifua hasa waweze kuwa wepesi na kwendana na kasi ya Emerson.

Lakini pia, Maximo na wasaidizi wake, Leonardo Neiva, Juma Pondamali, Salvatory Edward na Shadrack Nsajigwa, wanapaswa kuwa wakali katika kusimamia suala zima la upokeaji na utoaji pasi kwa kasi bila kuremba au kupoozesha mchezo kama atakavyo Emerson.

Emerson ametua nchini kujaribu bahati yake ya kusajiliwa na Yanga, ikiwa ni baada ya Mbrazil mwingine, Geilson Santos ‘Jaja’ kujiengua mwenyewe katika kikosi hicho kutokana na alichodai kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.

Jaja aliyetua Yanga Julai mwaka huu, alijipatia umaarufu baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Azam Septemba 14, mwaka huu katika mchezo wa Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kati ya mabao yake hayo, la pili alilifunga kwa ustadi mkubwa ambapo baada ya kumwomba Ngassa amwekee mpira kwenye njia na winga huyo kufanya hivyo, Mbrazil huyo alimchungulia kipa wa Azam, Mwadini Ally na kuubetua mpira uliopita juu yake na kutinga nyavuni.

Bao hilo dhidi ya Azam katika mchezo uliokuwa ukitabiriwa kuwa mgumu zaidi kwa Yanga, lilimfanya Jaja kujipatia umaarufu wa aina yake, lakini alijikuta akishindwa kuwateka mashabiki Ligi Kuu Tanzania Bara ilipoanza kutokana na kuambulia bao moja tu katika mechi saba.-bingwa






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4