Michepuko yasababisha ukatili
KUKITHIRI kwa matukio ya unyanyasaji kwa akina mama
kunasababisha baadhi ya wanaume kuwa na wapenzi wengine nje ya ndoa.
Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Jinsia na Uhamasishaji
kwa Jamii kutoka Shirika la Agape Aids Control Programme, Mustapha Isabuda.
Alisema katika utafiti wao, wamebaini kuwa sababu kubwa ya
wanaume wengi kutelekeza familia zao ni kutokana na kuendekeza michepuko,
kitendo ambacho wanawake wanabaki kuwa na mzigo mkubwa wa kulea watoto.
“Wanaume acheni michepuko, hii ndiyo sababu kubwa ya
familia nyingi kuvunjika, takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia Januari hadi Oktoba,
mwaka huu, jumla ya akina mama 274 kutoka halmashauri ya Kishapu na Shinyanga wamefanyiwa
ukatili wa kijinsia.
“Kutokana na ukatili wa kijinsia, jumla ya watoto 637
wamekosa haki zao za msingi kama elimu, chakula, malazi, matibabu na ustawi wao
kwa ujumla kutokana na kina baba kuwatelekeza wake zao,” alisema Isabuda.
Naye Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Shirika hilo,
Deozawadi Marandu, alisema miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo katika
mradi huo ni kuzuia mimba na ndoa za utotoni.-Mtanzania
|
Maoni
Chapisha Maoni