Maximo amtaka Traore wa El Merreikh
KOCHA wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo, ameutaka
uongozi wa klabu hiyo kufanya kila linalowezekana kumsajili mshambuliaji raia
wa Mali, Mohamed Traore, anayekipiga katika klabu ya El Merreikh ya Sudan.
Traore ametokea kuzivutia klabu kadhaa ambazo
zinaiwania saini yake, ikiwamo Azam ya Tanzania inayodaiwa kuanza mazungumzo
naye.
Mohamed Traore |
Habari kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, zinasema
kuwa Maximo anamtaka mshambuliaji huyo ili kuziba nafasi ya Mbrazil mwenzake,
Geilson Santos ‘Jaja’ aliyejiengua kutokana na kile alichodai kukabiliwa na
matatizo ya kifamilia.
Japo Maximo ametua nchini na Emerson Oliveira Neves
Rogue, bado atakuwa akihitaji mshambuliaji mahiri wa kati kwani Mbrazil huyo ni
kiungo.
Pamoja na kiu yake ya kumnasa Traore, bado Maximo
hana uhakika wa hilo kwani mshambuliaji huyo analipwa fedha nyingi mno na El
Merreikh hivyo Yanga watatakiwa ‘kuvunja benki’ kumng’oa katika klabu hiyo ya
Sudan.
“Kocha amesema anamtaka Traore, sijui itakuwaje
kwani kama unavyofahamu, Azam nao wanamtaka, ngoja tusubiri kuona nani
atakayeibuka kidedea,”
Imeelezwa kuwa iwapo Traore atatua Yanga, klabu hiyo
itamfyeka mchezaji mmoja wa kigeni kati ya Mnyarwanda Haruna Niyonzima na
Mganda Hamis Kiiza.
Traore imeelezwa kwa sasa analipwa dola za Marekani
180,000 (Sh milioni 300) kwa mwaka na El Merreikh mbali ya mshahara wa Dola za
Marekani 10,000 (Sh milioni 17,000).
Pamoja na kulipwa dau hilo, imeelezwa Traore amechoshwa
na maisha ndani ya klabu hiyo na kwamba yupo tayari kuichezea timu yoyote
Maoni
Chapisha Maoni