CHIPUKIZI:Wasanii wanashindwa kuwatumia mameneja

Displaying DSC_0727.JPG

‘Belays'


Displaying DSC_0731.JPG

Abel Gabriel:SANAA ya muziki wa Tanzania inazidi kukua na kutanuka kila siku na ndio maana kukicha inazidi kujinyakulia umaarufu nchini huku idadi ya wafuasi wake ikizidi kuoongezeka licha ya kukumbana na changamoto.  

Leo tunaye msanii chipukizi wa miondoko ya Rap Abel Gabriel ‘Belays’ mwenye ndoto za kuja kuwa staa mkubwa kwenye muziki huu.Tangu akiwa shule ya msingi huko mkoani Kigoma hadi sasa ana nyimbo tatu mkononi ambazo ni ‘Niwe nawe, Hujachelewa aliyoirekodi kwenye studio za Say Rekodi na ile ya ‘Waweza kwenda aliyoirekodi kwenye studio za Pamoja Records ambazo alianza kurekodi rasmi mwaka huu.  

Belays anasema kuwa licha ya mameneja kuwa tatizo kubwa kwao kutokana na kushindwa kuwapata lakini anadai kuwa wasanii wengi wanapowapata wasimamizi hao (meneja), wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kutokana na kutokuelewa namna ya kuwatumia meneja huo kwani wengi hushia kunyonywa tu na hao mameneja.  

“Wasanii wengi tunashindwa kufikia kilele cha mafaniko ya ndoto yetu kimuziki kutokana aina ya wasimamizi tunaowapata kutumia nafasi yetu ya umaskini kutukandamiza, hali hiyo inasababisha wasanii tufe maskini bila ya kuwa na chochote.

Wasanii wengi tunashindwa kufikia kilele cha mafaniko ya ndoto yetu kimuziki kutokana aina ya wasimamizi tunaowapata kutumia nafasi yetu ya umaskini kutukandamiza, hali hiyo inasababisha wasanii tufe maskini bila ya kuwa na chochote.

 “Kutokana na mazingira magumu ambayo wasimamizi wengi (mameneja), wanatukuta nayo ndiyo maana tunakuwa hatufanikiwi kwani mameneja wanakuwa wanataka kutumia hali yako ya kutokuwa nacho kukunyonya vya kutosha ambapo malipo yake kwako yanakuwa ni kukununulia nguo hata ikitokea kuna shoo meneje anakuwa anapata fungu kubwa kuliko wewe huku akiwa bado anakupangia hali inayorudisha nyuma kimuziki,” anasema.
Anasema anahitaji mtu aliye tayari(meneja) kwa ajili ya kufanya naye kazi kwa kuwa an akipaji chake na ndoto yake ni kuona siku mmoja muziki watanzania ukipiga hatua zaidi duniani kama ilivyo kwa mataifa yaliyoendelea ikiwemo Marekani.ambapo unaweza kuwasiliana nae kupitia kwenye 0782333029 +whatsapp,facebook: belyz gabriel baliko na instagram: belayz_gabriel.


we ni chipukizi wa muziki,filamu na hata mitindo na ungependa kuwa hapa mawasiliano ni haya +255767580313

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HADITHI:MWALIMU MAGDALENA sehemu ya 1

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 5

Hadithi: Mwalimu Magdalena sehemu ya 4